Jeremiah 28:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwaka uleule, mnamo mwezi wa tano wa mwaka wa nne wa utawala wa Sedekia mfalme wa Yuda, Hanania mwana wa Azuri, nabii kutoka mji wa Gibeoni, alisema nami katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Alisema nami mbele ya makuhani na watu wote, akaniambia,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika mwezi wa tano wa mwaka ule ule, yaani mwaka wa nne, mwanzoni mwa utawala wa Sedekia mfalme wa Yuda, nabii Hanania mwana wa Azuri, ambaye alitoka Gibeoni, akaniambia katika nyumba ya Mwenyezi Mungu mbele ya makuhani na watu wote:
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa, katika mwaka ule ule, mwanzo wa kutawala kwake Sedekia, mfalme wa Yuda, mwaka wa nne, mwezi wa tano, Hanania, mwana wa Azuri, nabii, wa Gibeoni, akasema nami ndani ya nyumba ya Bwana, mbele ya makuhani na watu wote, akisema,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwaka uleule, mnamo mwezi wa tano wa mwaka wa nne wa utawala wa Sedekia mfalme wa Yuda, Hanania mwana wa Azuri, nabii kutoka mji wa Gibeoni, alisema nami katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Alisema nami mbele ya makuhani na watu wote, akaniambia,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika mwezi wa tano wa mwaka ule ule, yaani mwaka wa nne, mwanzoni mwa utawala wa Sedekia mfalme wa Yuda, nabii Hanania mwana wa Azuri, ambaye alitoka Gibeoni, akaniambia katika nyumba ya BWANA mbele ya makuhani na watu wote:
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika mwezi wa tano wa mwaka ule ule, yaani mwaka wa nne, mwanzoni mwa utawala wa Sedekia mfalme wa Yuda, nabii Hanania mwana wa Azuri, ambaye alitoka Gibeoni, akaniambia katika nyumba ya bwana mbele ya makuhani na watu wote:
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa, katika mwaka ule ule, mwanzo wa kutawala kwake Sedekia, mfalme wa Yuda, mwaka wa nne, mwezi wa tano, Hanania, mwana wa Azuri, nabii, wa Gibeoni, akasema nami ndani ya nyumba ya BWANA, mbele ya makuhani na watu wote, akisema,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwaka uleule, mnamo mwezi wa tano wa mwaka wa nne wa utawala wa Sedekia mfalme wa Yuda, Hanania mwana wa Azuri, nabii kutoka mji wa Gibeoni, alisema nami katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Alisema nami mbele ya makuhani na watu wote, akaniambia,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa mwaka uleule, ufalme wa Sedekia, mfalme wa Yuda, ulipoanzia, katika mwezi wa tano wa mwaka wa nne, ndipo, mfumbuaji Hanania, mwana wa Azuri wa Gibeoni, aliponiambia Nyumbani mwa Bwana machoni pao watambikaji napo pao wote wa ukoo huu kwamba:
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa, katika mwaka ule ule, mwanzo wa kutawala kwake Sedekia, mfalme wa Yuda, mwaka wa nne, mwezi wa tano, Hanania, mwana wa Azuri, nabii, wa Gibeoni, akasema nami ndani ya nyumba ya BWANA, mbele ya makuhani na watu wote, akisema,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika mwaka uleule, maana yake mwaka wa ine wa utawala wa mufalme Zedekia juu ya Yuda, katika mwezi wa tano, Hanania, mwana wa Azuri, nabii kutoka muji Gibeoni, alisema nami katika nyumba ya Yawe. Alisema nami mbele ya makuhani na watu wote, akiniambia kwamba