Jeremiah 28:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye Hanania akasema hivi mbele ya watu wote, “Mwenyezi-Mungu asema: Hivi ndivyo nitakavyovunja nira ambayo mfalme Nebukadneza ameyavisha mataifa yote; nitafanya hivyo mnamo miaka miwili ijayo.” Kisha nabii Yeremia akaenda zake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
naye akasema mbele ya watu wote, “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: ‘Vivi hivi ndivyo nitakavyoivunja nira ya Nebukadneza mfalme wa Babeli kutoka shingo za mataifa katika muda huu wa miaka miwili.’ ” Alipofanya hivi, nabii Yeremia akaondoka zake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Hanania akanena mbele ya watu wote, akisema, Bwana asema hivi, Hivyo ndivyo nitakavyoivunja nira ya Nebukadreza, mfalme wa Babeli, kabla haujatimia muda wa miaka miwili mizima, na kuiondoa shingoni mwa mataifa yote. Basi nabii Yeremia akaenda zake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye Hanania akasema hivi mbele ya watu wote, “Mwenyezi-Mungu asema: Hivi ndivyo nitakavyovunja nira ambayo mfalme Nebukadneza ameyavisha mataifa yote; nitafanya hivyo mnamo miaka miwili ijayo.” Kisha nabii Yeremia akaenda zake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
naye akasema mbele ya watu wote, “Hili ndilo asemalo BWANA: ‘Vivi hivi ndivyo nitakavyoivunja nira ya Nebukadneza mfalme wa Babeli kutoka kwenye shingo za mataifa katika muda huu wa miaka miwili.’ ” Kwa jambo hili, nabii Yeremia akaondoka zake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
naye akasema mbele ya watu wote, “Hili ndilo asemalo bwana: ‘Vivi hivi ndivyo nitakavyoivunja nira ya Nebukadneza mfalme wa Babeli kutoka kwenye shingo za mataifa katika muda huu wa miaka miwili.’ ” Alipofanya hivi, nabii Yeremia akaondoka zake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Hanania akanena mbele ya watu wote, akisema, BWANA asema hivi, Hivyo ndivyo nitakavyoivunja nira ya Nebukadneza, mfalme wa Babeli, kabla haujatimia muda wa miaka miwili kamili, na kuiondoa shingoni mwa mataifa yote. Basi nabii Yeremia akaenda zake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye Hanania akasema hivi mbele ya watu wote, “Mwenyezi-Mungu asema: Hivi ndivyo nitakavyovunja nira ambayo mfalme Nebukadneza ameyavisha mataifa yote; nitafanya hivyo mnamo miaka miwili ijayo.” Kisha nabii Yeremia akaenda zake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Hanania akasema, watu wote wa ukoo huu wakimtazama, kwamba: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Hivi ndivyo, nitakavyoyavunja makongwa ya Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, shingoni pa mataifa yote, miaka miwili itakapopita. Kisha mfumbuaji Yeremia akashika njia kwenda zake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Hanania akanena mbele ya watu wote, akisema, BWANA asema hivi, Hivyo ndivyo nitakavyoivunja nira ya Nebukadreza, mfalme wa Babeli, kabla haujatimia muda wa miaka miwili mizima, na kuiondoa shingoni mwa mataifa yote. Basi nabii Yeremia akaenda zake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye Hanania akasema hivi mbele ya watu wote: Yawe anasema hivi: Mbele ya miaka miwili, hivi ndivyo nitakavyovunja nira ambayo mufalme Nebukadneza anayoibebesha mataifa yote. Kisha nabii Yeremia akajiendea.