Jeremiah 28:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, nasema kuwa nimeweka nira ya chuma ya utumwa shingoni mwa mataifa haya yote, nayo yatamtumikia Nebukadneza, mfalme wa Babuloni. Nimempa Nebukadneza hata wanyama wa porini wamtumikie.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli: Nitaweka nira ya chuma kwenye shingo za mataifa haya yote ili kufanya yamtumikie Nebukadneza mfalme wa Babeli, nao watamtumikia. Pia nitampa kutawala hata wanyama pori.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nimetia nira ya chuma juu ya shingo ya mataifa haya yote, ili wamtumikie Nebukadreza, mfalme wa Babeli nao watamtumikia; nami nimempa wanyama wa nchi pia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, nasema kuwa nimeweka nira ya chuma ya utumwa shingoni mwa mataifa haya yote, nayo yatamtumikia Nebukadneza, mfalme wa Babuloni. Nimempa Nebukadneza hata wanyama wa porini wamtumikie.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: Nitaweka nira ya chuma kwenye shingo za mataifa haya yote ili kufanya yamtumikie Nebukadneza mfalme wa Babeli, nao watamtumikia. Nitampa kutawala hata wanyama wa mwituni.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hili ndilo asemalo bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: Nitaweka nira ya chuma kwenye shingo za mataifa haya yote ili kufanya yamtumikie Nebukadneza mfalme wa Babeli, nao watamtumikia. Nitampa kutawala hata wanyama wa mwituni.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nimetia nira ya chuma juu ya shingo ya mataifa haya yote, ili wamtumikie Nebukadneza, mfalme wa Babeli nao watamtumikia; nami nimempa wanyama wa nchi pia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, nasema kuwa nimeweka nira ya chuma ya utumwa shingoni mwa mataifa haya yote, nayo yatamtumikia Nebukadneza, mfalme wa Babuloni. Nimempa Nebukadneza hata wanyama wa porini wamtumikie.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, anavyosema: Makongwa ya chuma nimetia shingoni pao haya mataifa yote, wamtumikie Nebukadinesari, mfalme wa Babeli; watamtumikia kweli, nao nyama wa porini nimempa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nimetia nira ya chuma juu ya shingo ya mataifa haya yote, ili wamtumikie Nebukadreza, mfalme wa Babeli nao watamtumikia; nami nimempa wanyama wa nchi pia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Nimeweka nira ya chuma ya utumwa kwenye shingo la mataifa yote ya pande hizi, yakuwe katika utumwa, nayo yatamutumikia Nebukadneza, mufalme wa Babeli. Nimemupa Nebukadneza hata nyama wa pori wamutumikie.