Jeremiah 28:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mnamo miaka miwili nitavirudisha hapa vyombo vyote vya nyumba ya Mwenyezi-Mungu ambavyo Nebukadneza, mfalme wa Babuloni alivichukua na kuvipeleka Babuloni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika muda wa miaka miwili nitavirudisha mahali hapa vyombo vyote vya nyumba ya Mwenyezi Mungu ambavyo Nebukadneza mfalme wa Babeli aliviondoa kutoka hapa na kuvipeleka Babeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kabla haujatimia muda wa miaka miwili mizima, nitavirudisha mahali hapa vyombo vyote vya nyumba ya Bwana, ambavyo Nebukadreza, mfalme wa Babeli, aliviondoa katika mahali hapa, akavichukua mpaka Babeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mnamo miaka miwili nitavirudisha hapa vyombo vyote vya nyumba ya Mwenyezi-Mungu ambavyo Nebukadneza, mfalme wa Babuloni alivichukua na kuvipeleka Babuloni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika muda wa miaka miwili nitavirudisha mahali hapa vyombo vyote vya nyumba ya BWANA ambavyo Nebukadneza mfalme wa Babeli aliviondoa kutoka hapa na kuvipeleka Babeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika muda wa miaka miwili nitavirudisha mahali hapa vyombo vyote vya nyumba ya bwana ambavyo Nebukadneza mfalme wa Babeli aliviondoa kutoka hapa na kuvipeleka Babeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kabla haujatimia muda wa miaka miwili mizima, nitavirudisha mahali hapa vyombo vyote vya nyumba ya BWANA, ambavyo Nebukadneza, mfalme wa Babeli, aliviondoa kutoka mahali hapa, akavipeleka mpaka Babeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mnamo miaka miwili nitavirudisha hapa vyombo vyote vya nyumba ya Mwenyezi-Mungu ambavyo Nebukadneza, mfalme wa Babuloni alivichukua na kuvipeleka Babuloni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bado miaka miwili ndipo, mimi nitakapovirudisha mahali hapa vyombo vyote vya Nyumba ya Bwana, Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, alivyovichukua mahali hapa na kuvipeleka Babeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kabla haujatimia muda wa miaka miwili mizima, nitavirudisha mahali hapa vyombo vyote vya nyumba ya BWANA, ambavyo Nebukadreza, mfalme wa Babeli, aliviondoa katika mahali hapa, akavichukua mpaka Babeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mbele ya miaka miwili nitavirudisha hapa vyombo vyote vya nyumba ya Yawe ambavyo Nebukadneza, mufalme wa Babeli alivikamata na kuvipeleka Babeli.