Jeremiah 28:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Na iwe hivyo! Mwenyezi-Mungu na afanye hivyo. Mwenyezi-Mungu na ayatimize maneno uliyotabiri, avirudishe hapa vyombo vya nyumba ya Mwenyezi-Mungu kutoka Babuloni pamoja na watu wote waliohamishiwa huko.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akasema, “Amen! Mwenyezi Mungu na afanye hivyo! Mwenyezi Mungu na ayatimize maneno ya unabii uliyoyatoa kwa kuvirudisha mahali hapa kutoka Babeli vyombo vya nyumba ya Mwenyezi Mungu na watu wote walio uhamishoni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
naam, nabii Yeremia akasema, Amina, Bwana na atende hivi; Bwana ayatimize maneno yako uliyotabiri, kuvirudisha hapa vyombo vya nyumba ya Bwana na watu wote waliofungwa, toka Babeli, hata mahali hapa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Na iwe hivyo! Mwenyezi-Mungu na afanye hivyo. Mwenyezi-Mungu na ayatimize maneno uliyotabiri, avirudishe hapa vyombo vya nyumba ya Mwenyezi-Mungu kutoka Babuloni pamoja na watu wote waliohamishiwa huko.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akasema, “Amen! BWANA na afanye hivyo! BWANA na ayatimize maneno uliyotoa unabii kwa kuvirudisha mahali hapa kutoka Babeli vyombo vya nyumba ya BWANA pamoja na wote waliohamishwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akasema, “Amen! bwana na afanye hivyo! bwana na ayatimize maneno uliyotoa unabii kwa kuvirudisha mahali hapa kutoka Babeli vyombo vya nyumba ya bwana pamoja na wote waliohamishwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
naam, nabii Yeremia akasema, Amina, BWANA na atende hivi; BWANA ayatimize maneno yako uliyotabiri, kuvirudisha hapa vyombo vya nyumba ya BWANA na watu wote waliofungwa, toka Babeli, hadi mahali hapa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Na iwe hivyo! Mwenyezi-Mungu na afanye hivyo. Mwenyezi-Mungu na ayatimize maneno uliyotabiri, avirudishe hapa vyombo vya nyumba ya Mwenyezi-Mungu kutoka Babuloni pamoja na watu wote waliohamishiwa huko.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akasema mfumbuaji Yeremia: Amin, na yawe hivyo! Bwana na ayafanye hivyo akiyatimiza maneno yako, uliyoyafumbua, akivirudisha mahali hapa vyombo vya Nyumba ya Bwana nayo mateka yote toka Babeli!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
naam, nabii Yeremia akasema, Amina, BWANA na atende hivi; BWANA ayatimize maneno yako uliyotabiri, kuvirudisha hapa vyombo vya nyumba ya BWANA na watu wote waliofungwa, toka Babeli, hata mahali hapa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ikuwe hivyo! Yawe afanye hivyo. Yawe ayatimize maneno uliyotabiri, avirudishe hapa vyombo vya nyumba ya Yawe kutoka Babeli pamoja na watu wote waliohamishiwa huko.