Jeremiah 28:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Manabii waliotutangulia mimi na wewe, tangu zamani za kale, walitabiri kwamba vita, njaa na maradhi vitazikumba nchi nyingi na tawala kubwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tangu mwanzo, manabii waliokutangulia wewe na mimi walitabiri vita, maafa na tauni dhidi ya nchi nyingi na falme kubwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Manabii waliokuwako kabla ya zamani zangu, na zamani zako, walitabiri juu ya nchi nyingi, na juu ya falme kubwa, habari ya vita, na ya mabaya, na ya tauni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Manabii waliotutangulia mimi na wewe, tangu zamani za kale, walitabiri kwamba vita, njaa na maradhi vitazikumba nchi nyingi na tawala kubwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tangu mwanzo, manabii waliokutangulia wewe na mimi walitabiri vita, maafa na tauni dhidi ya nchi nyingi na falme kubwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tangu mwanzo, manabii waliokutangulia wewe na mimi walitabiri vita, maafa na tauni dhidi ya nchi nyingi na falme kubwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Manabii walionitangulia, na waliokutangulia, walitabiri habari za vita, na za mabaya na za tauni juu ya nchi nyingi, na juu ya falme kubwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Manabii waliotutangulia mimi na wewe, tangu zamani za kale, walitabiri kwamba vita, njaa na maradhi vitazikumba nchi nyingi na tawala kubwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wafumbuaji waliokuwa mbele yangu na mbele yako toka siku za kale walifumbulia nchi nyingi, hata nchi zenye wafalme wakuu vita na mabaya na magonjwa yauayo yatakayokuja.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Manabii waliokuwako kabla ya zamani zangu, na zamani zako, walitabiri juu ya nchi nyingi, na juu ya falme kubwa, habari ya vita, na ya mabaya, na ya tauni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Manabii waliotangulia mbele yetu, mimi na wewe, zamani za kale walitabiri kwamba vita, njaa na magonjwa makali vitazipata inchi nyingi na tawala kubwa.