Jeremiah 29:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nasema hivi: Tazama, ninawapelekea upanga, njaa na maradhi mabaya; nitawafanya kuwa kama tini mbaya sana, hata haziwezi kuliwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Naam, hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: “Nitatuma upanga, njaa na tauni dhidi yao, nami nitawafanya kuwa kama tini mbovu zilizooza, zisizofaa kuliwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana wa majeshi asema hivi, Tazama, nitaleta juu yao upanga, na njaa, na tauni, nami nitawafanya kuwa kama tini mbovu, zisizoweza kuliwa, kwa kuwa ni mbovu sana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nasema hivi: Tazama, ninawapelekea upanga, njaa na maradhi mabaya; nitawafanya kuwa kama tini mbaya sana, hata haziwezi kuliwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
naam, hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu Zote: “Nitatuma upanga, njaa na tauni dhidi yao nami nitawafanya kuwa kama tini dhaifu zile ambazo ni mbaya sana zisizofaa kuliwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Naam, hili ndilo asemalo bwana Mwenye Nguvu Zote: “Nitatuma upanga, njaa na tauni dhidi yao, nami nitawafanya kuwa kama tini dhaifu zile ambazo ni mbovu sana zisizofaa kuliwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA wa majeshi asema hivi, Tazama, nitaleta juu yao upanga, na njaa, na tauni, nami nitawafanya kuwa kama tini mbovu, zisizoweza kuliwa, kwa kuwa ni mbovu sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nasema hivi: Tazama, ninawapelekea upanga, njaa na maradhi mabaya; nitawafanya kuwa kama tini mbaya sana, hata haziwezi kuliwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema: Wataniona, nikituma kwao panga na njaa na magonjwa mabaya, nikiwageuza kuwa kuyu zitapishazo, zisizolika kwa ubaya wao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA wa majeshi asema hivi, Tazama, nitaleta juu yao upanga, na njaa, na tauni, nami nitawafanya kuwa kama tini mbovu, zisizoweza kuliwa, kwa kuwa ni mbovu sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitawatumia vita, njaa na magonjwa makali. Nitawafanya kuwa kama matunda mabaya sana ya tini zisizoweza hata kukuliwa.