Jeremiah 29:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitawaandama kwa upanga, njaa na maradhi mabaya. Nitawafanya kuwa kitu cha kuchukiza kwa tawala zote za dunia, naam, kitu cha laana, kioja, dharau na kitu cha kupuuzwa katika mataifa yote nilikowafukuzia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitawafukuza kwa upanga, kwa njaa na kwa tauni, nami nitawafanya kuwa chukizo kwa falme zote za dunia, kitu cha laana na cha kutisha, kisichofaa na cha kuzomewa miongoni mwa mataifa nitakakowafukuzia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nitawafuatia kwa upanga, na njaa, na tauni, nami nitawatoa watupwe huko na huko katika falme zote za dunia, wawe kitu cha kulaaniwa, na cha kushangaza, na cha kuzomewa, na cha kulaumiwa, katika mataifa yote nilikowafukuza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitawaandama kwa upanga, njaa na maradhi mabaya. Nitawafanya kuwa kitu cha kuchukiza kwa tawala zote za dunia, naam, kitu cha laana, kioja, dharau na kitu cha kupuuzwa katika mataifa yote nilikowafukuzia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitawafukuza kwa upanga, kwa njaa na kwa tauni nami nitawafanya kitu cha kuchukiza sana kwa falme zote za dunia na kuwa kitu cha laana na cha kuogofya, cha dharau na kukemewa, miongoni mwa mataifa yote nitakakowafukuzia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitawafukuza kwa upanga, kwa njaa na kwa tauni, nami nitawafanya kitu cha kuchukiza sana kwa falme zote za dunia, na kuwa kitu cha laana na cha kuogofya, cha dharau na kukemewa, miongoni mwa mataifa yote nitakakowafukuzia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nitawafuatia kwa upanga, na njaa, na tauni, nami nitawatoa watupwe huku na huko katika falme zote za dunia, wawe kitu cha kulaaniwa, na cha kushangaza, na cha kuzomewa, na cha kulaumiwa, katika mataifa yote nilikowafukuza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitawaandama kwa upanga, njaa na maradhi mabaya. Nitawafanya kuwa kitu cha kuchukiza kwa tawala zote za dunia, naam, kitu cha laana, kioja, dharau na kitu cha kupuuzwa katika mataifa yote nilikowafukuzia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nitawakimbiza kwa panga na kwa njaa na kwa magonjwa mabaya, nitawatoa, watupwe huko na huko katika nchi zote zenye wafalme huku ulimwenguni, waapizwe kwa kustukiwa, wazomelewe na kutukanwa kwenye mataifa yote, nitakakowatupa,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nitawafuatia kwa upanga, na njaa, na tauni, nami nitawatoa watupwe huko na huko katika falme zote za dunia, wawe kitu cha kulaaniwa, na cha kushangaza, na cha kuzomewa, na cha kulaumiwa, katika mataifa yote nilikowafukuza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitawashambulia kwa vita, njaa na magonjwa makali. Nitawafanya kuwa kitu cha kuchukiza kwa falme zote za dunia; nitawafanya kuwa mufano wa kutumia kwa kutoa laana. Mutakuwa kitu cha kushangaza, cha kuzarauliwa na cha kuzomewa kati ya mataifa yote nitakapowasambaza.