Jeremiah 29:23 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisa ni kwamba walitenda mambo ya aibu katika Israeli. Walizini na wake za jirani zao, na kusema maneno ya uongo kwa jina langu, jambo ambalo mimi sikuwaamuru walifanye. Mimi nayajua hayo; nimeyashuhudia. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa wamefanya mambo maovu kabisa katika Israeli, wamezini na wake za majirani zao, tena kwa Jina langu wamesema uongo, mambo ambayo sikuwaambia kuyafanya. Nami nayajua haya, na ni shahidi wa jambo hilo,” asema Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kwa sababu wametenda upumbavu katika Israeli, nao wamezini na wake za jirani zao, nao wamenena maneno ya uongo kwa jina langu, nisiyowaamuru; nami ndimi nijuaye, nami ni shahidi, asema Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisa ni kwamba walitenda mambo ya aibu katika Israeli. Walizini na wake za jirani zao, na kusema maneno ya uongo kwa jina langu, jambo ambalo mimi sikuwaamuru walifanye. Mimi nayajua hayo; nimeyashuhudia. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa wamefanya mambo maovu kabisa katika Israeli, wamezini na wake za majirani zao, tena kwa Jina langu wamesema uongo, mambo ambayo sikuwaambia kuyafanya, nami ni shahidi wa jambo hilo,” asema BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa wamefanya mambo maovu kabisa katika Israeli, wamezini na wake za majirani zao, tena kwa Jina langu wamesema uongo, mambo ambayo sikuwaambia kuyafanya. Nami nayajua haya, na ni shahidi wa jambo hilo,” asema bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kwa sababu wametenda upumbavu katika Israeli, nao wamezini na wake za jirani zao, nao wamenena maneno ya uongo kwa jina langu, nisiyowaamuru; nami ndimi nijuaye, nami ni shahidi, asema BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisa ni kwamba walitenda mambo ya aibu katika Israeli. Walizini na wake za jirani zao, na kusema maneno ya uongo kwa jina langu, jambo ambalo mimi sikuwaamuru walifanye. Mimi nayajua hayo; nimeyashuhudia. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa kuwa wamefanya yasiyofanywa kwao Waisiraeli, wakifanya ugoni na wanawake wa wenzao, wakasema neno la uwongo katika Jina langu, nami sikuwaagiza neno, Mimi ninayajua haya, ninayashuhudia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kwa sababu wametenda upumbavu katika Israeli, nao wamezini na wake za jirani zao, nao wamenena maneno ya uongo kwa jina langu, nisiyowaamuru; nami ndimi nijuaye, nami ni shahidi, asema BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Jambo hili litawafikia kwa sababu wametenda katika Israeli mambo yasiyofanyika. Walizini na wake za jirani zao, na kusema maneno ya uongo kwa jina langu, jambo ambalo mimi sikuwaamuru wafanye. Mimi ninajua hayo. Nimeyashuhudia. –Ni ujumbe wa Yawe.