Jeremiah 29:26 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
‘Mwenyezi-Mungu amekufanya wewe Sefania kuwa kuhani badala ya kuhani Yehoyada, uwe mkuu wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Ni wajibu wako kumtia gerezani na kumfunga minyororo mwendawazimu yeyote anayetabiri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
‘Mwenyezi Mungu amekuweka wewe uwe kuhani badala ya Yehoyada ili uwe msimamizi wa nyumba ya Mwenyezi Mungu. Unapaswa kumfunga kwa mikatale na mnyororo wa shingoni mwendawazimu yeyote anayejifanya nabii.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana amekufanya kuhani badala ya Yehoyada, kuhani, ili mpate kuwa watumishi katika nyumba ya Bwana, kwa kila mtu aliye na wazimu, na kwa kila mtu ajifanyaye kuwa nabii, umtie katika mkatale na pingu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
‘Mwenyezi-Mungu amekufanya wewe Sefania kuwa kuhani badala ya kuhani Yehoyada, uwe mkuu wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Ni wajibu wako kumtia gerezani na kumfunga minyororo mwendawazimu yeyote anayetabiri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
‘BWANA amekuweka wewe uwe kuhani badala ya Yehoyada uwe msimamizi wa nyumba ya BWANA, utamfunga kwa mikatale na mnyororo wa shingoni mwendawazimu ye yote anayejifanya nabii.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
‘ bwana amekuweka wewe uwe kuhani badala ya Yehoyada ili uwe msimamizi wa nyumba ya bwana. Unapaswa kufunga kwa mikatale na mnyororo wa shingoni mwendawazimu yeyote anayejifanya nabii.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA amekufanya kuhani badala ya Yehoyada, kuhani, ili mpate kuwa watumishi katika nyumba ya BWANA, kwa kila mtu aliye na wazimu, na kwa kila mtu ajifanyaye kuwa nabii, umtie katika mkatale na pingu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
‘Mwenyezi-Mungu amekufanya wewe Sefania kuwa kuhani badala ya kuhani Yehoyada, uwe mkuu wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Ni wajibu wako kumtia gerezani na kumfunga minyororo mwendawazimu yeyote anayetabiri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana amekuweka kuwa mtambikaji mahali pa mtambikaji Yoyada, mwe wasimamizi Nyumbani mwa Bwana kuwaangalia wote wenye wazimu nao wajiwaziao kuwa wafumbuaji, uwafunge mikatale na mapingu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA amekufanya kuhani badala ya Yehoyada, kuhani, ili mpate kuwa watumishi katika nyumba ya BWANA, kwa kila mtu aliye na wazimu, na kwa kila mtu ajifanyaye kuwa nabii, umtie katika mkatale na pingu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe amekufanya wewe Zefania kuwa kuhani kwa pahali pa kuhani Yehoyada, kusudi ukuwe mukubwa wa nyumba ya Yawe. Wewe utashugulika na kumutia katika kifungo na kumufunga kwa minyororo mwenda-wazimu yeyote anayetabiri.