Jeremiah 29:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Oeni wake, mpate watoto; waozeni wana wenu na binti zenu nao pia wapate watoto. Ongezekeni na wala msipungue.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Oeni wake na mzae watoto wa kiume na wa kike; watafutieni wake watoto wenu wa kiume, na waozeni binti zenu ili nao wazae watoto wa kiume na wa kike; mkaongezeke huko, wala msipungue idadi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
oeni wake, mkazae wana na binti; kawaozeni wake wana wenu, mkawaoze waume binti zenu, wazae wana na binti; mkaongezeke huko wala msipungue.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Oeni wake, mpate watoto; waozeni wana wenu na binti zenu nao pia wapate watoto. Ongezekeni na wala msipungue.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Oeni wake na mzae wana na binti, waozeni wana wenu wake nanyi watoeni binti zenu waolewe, ili nao pia wazae wana na binti. Ongezekeni idadi yenu huko, wala msipungue.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Oeni wake na mzae wana na binti, waozeni wana wenu wake, nanyi watoeni binti zenu waolewe, ili nao pia wazae wana na binti. Ongezekeni idadi yenu huko, wala msipungue.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
oeni wake, mkazae wana na binti; kawaozeni wake wana wenu, mkawaoze waume binti zenu, wazae wana na binti; mkaongezeke huko wala msipungue.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Oeni wake, mpate watoto; waozeni wana wenu na binti zenu nao pia wapate watoto. Ongezekeni na wala msipungue.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Oeni wanawake, mzae watoto wa kiume na wa kike! Nao wana wenu wa kiume wapatieni wanawake, nao wana wenu wa kike mwaoze waume, wazae watoto wa kiume na wa kike, mwe wengi huko, msipunguke!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
oeni wake, mkazae wana na binti; kawaozeni wake wana wenu, mkawaoze waume binti zenu, wazae wana na binti; mkaongezeke huko wala msipungue.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muoe, mupate watoto. Muwaoee wana wenu na kuowesha wabinti zenu, nao vilevile wapate watoto. Muongezeke kule wala musipunguke.