Jeremiah 3:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mume akimpa talaka mkewe, naye akaondoka kwake, na kuwa mke wa mwanamume mwingine, je mume yule aweza kumrudia mwanamke huyo? Je, kufanya hivyo hakutaitia nchi unajisi mkubwa? Wewe Israeli, umefanya ukahaba na wapenzi wengi, je, sasa unataka kunirudia mimi?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kama mtu akimpa talaka mkewe, naye akamwacha na akaolewa na mtu mwingine, je, huyo mume aweza kumrudia tena? Je, hiyo nchi haitanajisika kabisa? Lakini umeishi kama kahaba na wapenzi wengi: Je, sasa utanirudia tena?” asema Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Watu husema, Mtu akimwacha mkewe, naye akienda zake, akawa mke wa mtu mwingine, je! Mtu huyo atamrudia tena? Je! Nchi hiyo haitatiwa unajisi? Lakini wewe umefanya mambo ya ukahaba na wapenzi wengi; nawe, je! Utanirudia mimi? Asema Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mume akimpa talaka mkewe, naye akaondoka kwake, na kuwa mke wa mwanamume mwingine, je mume yule aweza kumrudia mwanamke huyo? Je, kufanya hivyo hakutaitia nchi unajisi mkubwa? Wewe Israeli, umefanya ukahaba na wapenzi wengi, je, sasa unataka kunirudia mimi?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kama mtu akimpa talaka mkewe, naye akamwacha na akaolewa na mtu mwingine, je, huyo mume aweza kumrudia tena? Je, hiyo nchi haitanajisika kabisa? Lakini umeishi kama kahaba na wapenzi wengi: je, sasa utanirudia tena?” asema BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kama mtu akimpa talaka mkewe, naye akamwacha na akaolewa na mtu mwingine, je, huyo mume aweza kumrudia tena? Je, hiyo nchi haitanajisika kabisa? Lakini umeishi kama kahaba na wapenzi wengi: je, sasa utanirudia tena?” asema bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Watu husema, Mtu akimwacha mkewe, naye akienda zake, akawa mke wa mtu mwingine, je! Mtu huyo atamrudia tena? Je! Nchi hiyo haitatiwa unajisi? Lakini wewe umefanya mambo ya ukahaba na wapenzi wengi; nawe, je! Utanirudia mimi? Asema BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mume akimpa talaka mkewe, naye akaondoka kwake, na kuwa mke wa mwanamume mwingine, je mume yule aweza kumrudia mwanamke huyo? Je, kufanya hivyo hakutaitia nchi unajisi mkubwa? Wewe Israeli, umefanya ukahaba na wapenzi wengi, je, sasa unataka kunirudia mimi?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akasema: Kama mtu anampa mkewe ruhusa, ajiendee, naye akatoka kwake, akawa wa mume mwingine, je? Yule wa kwanza atamrudia? Nchi ile isingepata uchafu? Nawe wewe umezini na wenzio wengi, kisha unirudie mimi! ndivyo, asemavyo Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Watu husema, Mtu akimwacha mkewe, naye akienda zake, akawa mke wa mtu mwingine, je! Mtu huyo atamrudia tena? Je! Nchi hiyo haitatiwa unajisi? Lakini wewe umefanya mambo ya ukahaba na wapenzi wengi; nawe, je! Utanirudia mimi? Asema BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mume akiachana na muke wake, naye muke akijiendea, na kuolewa na mwingine, mume yule anaweza kumurudilia muke huyo? Kufanya hivyo hakutaichafua inchi kabisa? Wewe Israeli, umefanya ukahaba na wapenzi wengi, sasa unataka kunirudilia mimi? –Ni ujumbe wa Yawe.–