Jeremiah 3:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wewe, kiri tu kosa lako: Kwamba umeniasi mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako; kwamba chini ya kila mti wenye majani, umewapa miungu wengine mapenzi yako wala hukuitii sauti yangu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ungama dhambi zako tu: kwamba umemwasi Mwenyezi Mungu, Mungu wako, umetapanya wema wako kwa miungu ya kigeni chini ya kila mti unaotanda, nawe hukunitii mimi,’ ” asema Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ungama uovu wako tu; ya kwamba umemwasi Bwana, Mungu wako, na njia zako zimekuwa nyingi kuwaendea wageni chini ya kila mti wenye majani mabichi, wala hamkuitii sauti yangu, asema Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wewe, kiri tu kosa lako: kwamba umeniasi mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako; kwamba chini ya kila mti wenye majani, umewapa miungu wengine mapenzi yako wala hukuitii sauti yangu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ungama dhambi zako tu: kwamba umemwasi BWANA Mungu wako, umetapanya wema wako kwa miungu ya kigeni chini ya kila mti unaotanda, nawe hukunitii mimi,’ ” asema BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ungama dhambi zako tu: kwamba umemwasi bwana Mwenyezi Mungu wako, umetapanya wema wako kwa miungu ya kigeni chini ya kila mti unaotanda, nawe hukunitii mimi,’ ” asema bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ungama uovu wako tu; ya kwamba umemwasi BWANA, Mungu wako, na njia zako zimekuwa nyingi kuwaendea wageni chini ya kila mti wenye majani mabichi, wala hamkuitii sauti yangu, asema BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wewe, kiri tu kosa lako: Kwamba umeniasi mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako; kwamba chini ya kila mti wenye majani, umewapa miungu wengine mapenzi yako wala hukuitii sauti yangu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jua tu, ya kuwa umekora manza ulipomtengua Bwana Mungu wako ukienda huko na huko kufuata wageni chini ya kila mti wenye majani mengi, lakini sauti yangu hukuisikia; ndivyo, asemavyo Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ungama uovu wako tu; ya kwamba umemwasi BWANA, Mungu wako, na njia zako zimekuwa nyingi kuwaendea wageni chini ya kila mti wenye majani mabichi, wala hamkuitii sauti yangu, asema BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wewe, kubali tu kosa lako: kwamba umeniasi mimi Yawe, Mungu wako; kwamba chini ya kila muti wenye majani, umeonyesha mapenzi yako kwa miungu mingine, wala haukuitii sauti yangu. –Ni ujumbe wa Yawe.