Jeremiah 3:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Rudini, enyi watoto msio na uaminifu, maana, mimi ndimi Bwana wenu. Nitawachukua mmoja kutoka kila mji, na wawili kutoka katika kila ukoo, niwapeleke hadi mlimani Siyoni. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Rudini, enyi watu msio waaminifu, kwa kuwa mimi ni mume wenu,” asema Mwenyezi Mungu. “Nitawachagua ninyi, mmoja kutoka mji, na wawili kutoka ukoo, nami nitawaleta Sayuni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Rudini, enyi watoto wenye kuasi, asema Bwana; maana mimi ni mume wenu; nami nitatwaa mtu mmoja wa mji mmoja, na wawili wa jamaa moja, nami nitawaleta hata Sayuni;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Rudini, enyi watoto msio na uaminifu, maana, mimi ndimi Bwana wenu. Nitawachukua mmoja kutoka kila mji, na wawili kutoka katika kila ukoo, niwapeleke hadi mlimani Siyoni. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Rudini, enyi watu msio waaminifu, kwa kuwa mimi ni mume wenu,” asema BWANA. “Nitawachagua ninyi, mmoja kutoka kwenye mji na wawili kutoka kwenye ukoo, nami nitawaleta Sayuni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Rudini, enyi watu msio waaminifu, kwa kuwa mimi ni mume wenu,” asema bwana. “Nitawachagua ninyi, mmoja kutoka kwenye mji, na wawili kutoka kwenye ukoo, nami nitawaleta Sayuni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Rudini, enyi watoto wenye kuasi, asema BWANA; maana mimi ni mume wenu; nami nitatwaa mtu mmoja wa mji mmoja, na wawili wa jamaa moja, nami nitawaleta hadi Sayuni;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Rudini, enyi watoto msio na uaminifu, maana, mimi ndimi Bwana wenu. Nitawachukua mmoja kutoka kila mji, na wawili kutoka katika kila ukoo, niwapeleke hadi mlimani Siyoni. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Rudini, ninyi wana mlioniacha! ndivyo, asemavyo Bwana. Kwani mimi ni bwana wenu; nitawachukua mmoja katika mji mmoja, tena wawili katika udugu mmoja, niwapeleke Sioni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Rudini, enyi watoto wenye kuasi, asema BWANA; maana mimi ni mume wenu; nami nitatwaa mtu mmoja wa mji mmoja, na wawili wa jamaa moja, nami nitawaleta hata Sayuni;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Murudi, enyi watoto musiokuwa na uaminifu, maana, mimi ndimi Bwana wenu. Nitawatwaa mumoja kutoka kila muji, na wawili kutoka katika kila ukoo, niwapeleke mpaka kwenye mulima Sayuni. –Ni ujumbe wa Yawe.