Jeremiah 3:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu asema, “Israeli, mimi niliwaza, laiti ningekuweka miongoni mwa wanangu, na kukupa nchi nzuri ajabu, urithi usio na kifani kati ya mataifa yote. Nilidhani ungeniita, ‘Baba Yangu’, na kamwe usingeacha kunifuata.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mimi mwenyewe nilisema, “ ‘Tazama jinsi nitakavyowatunza kwa furaha kama wana na kuwapa nchi nzuri, urithi ulio mzuri kuliko wa taifa jingine lolote.’ Nilidhani mngeniita ‘Baba,’ na msingegeuka, mkaacha kunifuata.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini mimi nalisema, Nitawezaje kukuweka pamoja na watoto, na kukupa nchi ipendezayo, urithi ulio mwema wa mataifa? Nami nikasema, Mtaniita, Baba yangu, wala hamtageuka na kuacha kunifuata.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu asema, “Israeli, mimi niliwaza, laiti ningekuweka miongoni mwa wanangu, na kukupa nchi nzuri ajabu, urithi usio na kifani kati ya mataifa yote. Nilidhani ungeniita, ‘Baba Yangu’, na kamwe usingeacha kunifuata.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mimi mwenyewe nilisema, “ ‘Tazama jinsi nitakavyowatunza kwa furaha kama wana na kuwapa nchi nzuri, urithi ulio mzuri kuliko wa taifa jingine lo lote.’ Nilidhani mngeniita ‘Baba’ na kwamba msingegeuka, mkaacha kunifuata.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mimi mwenyewe nilisema, “ ‘Tazama jinsi nitakavyowatunza kwa furaha kama wana na kuwapa nchi nzuri, urithi ulio mzuri kuliko wa taifa jingine lolote.’ Nilidhani mngeniita ‘Baba,’ na msingegeuka, mkaacha kunifuata.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini mimi nilisema, Nitawezaje kukuweka pamoja na watoto, na kukupa nchi ipendezayo, urithi ulio mwema wa mataifa? Nami nikasema, Mtaniita, Baba yangu, wala hamtageuka na kuacha kunifuata.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu asema, “Israeli, mimi niliwaza, laiti ningekuweka miongoni mwa wanangu, na kukupa nchi nzuri ajabu, urithi usio na kifani kati ya mataifa yote. Nilidhani ungeniita, ‘Baba Yangu’, na kamwe usingeacha kunifuata.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nami nalisema: A, nitakuweka kwenye wana, nitakupa nchi ya kupendezwa nayo kwa kuwa yenye utukufu kuyapita matukufu yote ya wamizimu! Nikasema: Utaniita: Baba! Usiondoke nyuma yangu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini mimi nalisema, Nitawezaje kukuweka pamoja na watoto, na kukupa nchi ipendezayo, urithi ulio mwema wa mataifa? Nami nikasema, Mtaniita, Baba yangu, wala hamtageuka na kuacha kunifuata.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe anasema: Wewe Israeli, mimi niliwaza hivi: heri ningekuhesabia kati ya wana wangu, na kukupa inchi nzuri ajabu, ndio urizi unaopita inchi zote za mataifa. Nilizani utaniita Baba Yako, na kwamba haungeacha kunifuata.