Jeremiah 3:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Inua macho uvitazame vilele vya vilima! Pako wapi mahali ambapo hawajalala nawe? Uliwangoja wapenzi wako kando ya njia, kama bedui aviziavyo watu jangwani. Umeifanya nchi kuwa najisi, kwa ukahaba wako mbaya kupindukia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Inua macho utazame miinuko iliyo kame na uone. Je, pana mahali ambapo hawajalala nawe? Uliketi kando ya barabara ukiwasubiri wapenzi, ukakaa kama mtu anayehamahama jangwani. Umeinajisi nchi kwa ukahaba wako na uovu wako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Inua macho yako, ukavitazame vilele vya milima, ukaone; pa wapi mahali ambapo hawakulala nawe? Kando ya njia umeketi ili kuwangojea, kama vile Mwarabu jangwani; nawe umeitia nchi unajisi kwa ukahaba wako na uovu wako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Inua macho uvitazame vilele vya vilima! Pako wapi mahali ambapo hawajalala nawe? Uliwangoja wapenzi wako kando ya njia, kama bedui aviziavyo watu jangwani. Umeifanya nchi kuwa najisi, kwa ukahaba wako mbaya kupindukia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Inua macho utazame miinuko iliyo kame na uone. Je, pana mahali ambapo hawajalala nawe? Uliketi kando ya barabara ukiwasubiri wapenzi, ukakaa kama yeye ahamahamaye jangwani. Umeinajisi nchi kwa ukahaba wako na uovu wako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Inua macho utazame miinuko iliyo kame na uone. Je, pana mahali ambapo hawajalala nawe? Uliketi kando ya barabara ukiwasubiri wapenzi, ukakaa kama yeye ahamahamaye jangwani. Umeinajisi nchi kwa ukahaba wako na uovu wako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Inua macho yako, ukavitazame vilele vya milima, ukaone; pako wapi mahali ambapo hawakulala nawe? Kando ya njia umeketi ili kuwangojea, kama vile Mwarabu jangwani; nawe umeitia nchi unajisi kwa ukahaba wako na uovu wako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Inua macho uvitazame vilele vya vilima! Pako wapi mahali ambapo hawajalala nawe? Uliwangoja wapenzi wako kando ya njia, kama bedui aviziavyo watu jangwani. Umeifanya nchi kuwa najisi, kwa ukahaba wako mbaya kupindukia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yaelekeze macho yako vilimani, utazame! Pako mahali, usipofanyiziwa ugoni? Ulikaa njiani na kuwangoja kama Mwarabu nyikani, ukaichafua nchi kwa ugoni wako uliokuwa mbaya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Inua macho yako, ukavitazame vilele vya milima, ukaone; pa wapi mahali ambapo hawakulala nawe? Kando ya njia umeketi ili kuwangojea, kama vile Mwarabu jangwani; nawe umeitia nchi unajisi kwa ukahaba wako na uovu wako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Inua macho, uangalie vilele vya vilima! Kuna nafasi ambapo hawajalala nawe? Uliwangoja wapenzi wako kando ya njia, kama mubedui anavyovizia watu katika jangwa. Umeichafua inchi kwa ukahaba wako mubaya sana.