Jeremiah 3:22 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Rudini, enyi watoto msio na uaminifu, mimi nitaponya utovu wenu wa uaminifu. “Nanyi mwasema: ‘Tazama, sisi tunarudi kwako, maana, wewe ndiwe Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Rudini, enyi watu msio waaminifu, nami nitawaponya ukengeufu wenu.” “Naam, tutakuja kwako, kwa maana wewe ni Mwenyezi Mungu, Mungu wetu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Rudini, enyi watoto waasi, mimi nitaponya maasi yenu. Tazama, tumekuja kwako; maana wewe u Bwana, Mungu wetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Rudini, enyi watoto msio na uaminifu, mimi nitaponya utovu wenu wa uaminifu. “Nanyi mwasema: ‘Tazama, sisi tunarudi kwako, maana, wewe ndiwe Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Rudini, enyi watu msio waaminifu, nami nitawaponya ukengeufu wenu.” “Naam, tutakujia kwa maana wewe ni BWANA Mungu wetu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Rudini, enyi watu msio waaminifu, nami nitawaponya ukengeufu wenu.” “Naam, tutakuja kwako, kwa maana wewe ni bwana Mwenyezi Mungu wetu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Rudini, enyi watoto waasi, mimi nitaponya maasi yenu. Tazama, tumekuja kwako; maana wewe u BWANA, Mungu wetu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Rudini, enyi watoto msio na uaminifu, mimi nitaponya utovu wenu wa uaminifu. “Nanyi mwasema: ‘Tazama, sisi tunarudi kwako, maana, wewe ndiwe Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Rudini, ninyi wana mlioniacha! Nitawaponya, ingawa mmeniacha. Tutazame! Tumekujia, kwani wewe ndiwe Bwana Mungu wetu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Rudini, enyi watoto waasi, mimi nitaponya maasi yenu. Tazama, tumekuja kwako; maana wewe u BWANA, Mungu wetu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Murudi, enyi watoto musiokuwa na uaminifu, mimi nitawaponyesha ukosefu wenu wa uaminifu. Nanyi munasema: Sisi tunarudi kwako, maana wewe ndiwe Yawe, Mungu wetu.