Jeremiah 3:25 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hatuna budi kujilaza chini kwa aibu, na kuiacha fedheha yetu itufunike. Tangu ujana wetu hadi leo hii, wazee wetu na sisi wenyewe tumetenda dhambi mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, wala hatukumtii Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sisi na tulale chini katika aibu yetu, na fedheha yetu itufunike. Tumetenda dhambi dhidi ya Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, sisi na mababa zetu; tangu ujana wetu hadi leo hatukumtii Mwenyezi Mungu, Mungu wetu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na tulale kwa aibu yetu, haya yetu na itufunike; kwa maana tumemwasi Bwana, Mungu wetu, sisi na baba zetu, tangu ujana wetu hata leo; wala hatukuitii sauti ya Bwana, Mungu wetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hatuna budi kujilaza chini kwa aibu, na kuiacha fedheha yetu itufunike. Tangu ujana wetu hadi leo hii, wazee wetu na sisi wenyewe tumetenda dhambi mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, wala hatukumtii Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sisi na tulale chini katika aibu yetu, fedheha yetu na itufunike. Tumetenda dhambi dhidi ya BWANA Mungu wetu, sisi na mababa zetu; tangu ujana wetu hadi leo hatukumtii BWANA Mungu wetu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sisi na tulale chini katika aibu yetu, na fedheha yetu itufunike. Tumetenda dhambi dhidi ya bwana Mwenyezi Mungu wetu, sisi na mababa zetu; tangu ujana wetu hadi leo hatukumtii bwana Mwenyezi Mungu wetu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na tulale kwa aibu yetu, haya yetu na itufunike; kwa maana tumemwasi BWANA, Mungu wetu, sisi na baba zetu, tangu ujana wetu hata leo; wala hatukuitii sauti ya BWANA, Mungu wetu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hatuna budi kujilaza chini kwa aibu, na kuiacha fedheha yetu itufunike. Tangu ujana wetu hadi leo hii, wazee wetu na sisi wenyewe tumetenda dhambi mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, wala hatukumtii Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sharti tulale kwa kupatwa na soni, nayo matusi yatufunike, kwani tumemkosea Bwana Mungu wetu, sisi na baba zetu tangu utoto wetu mpaka siku hii ya leo, hatukuisikia sauti ya Bwana Mungu wetu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na tulale kwa aibu yetu, haya yetu na itufunike; kwa maana tumemwasi BWANA, Mungu wetu, sisi na baba zetu, tangu ujana wetu hata leo; wala hatukuitii sauti ya BWANA, Mungu wetu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sherti tujilaze chini kwa ajili ya haya, na kujiachilia kufunikiwa na haya yetu. Tangu ujana wetu mpaka leo hii, sisi wenyewe, kama vile babu zetu, tumetenda zambi mbele ya Yawe, Mungu wetu, wala hatukumutii Yawe, Mungu wetu.