Jeremiah 3:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati wa utawala wa mfalme Yosia, Mwenyezi-Mungu aliniambia hivi: “Je, umeona jinsi Israeli asiye mwaminifu alivyofanya? Aliniacha, akapanda juu ya kila kilima kirefu na kwenda chini ya kila mti wenye majani mabichi, akafanya ukahaba wake humo!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati wa utawala wa Mfalme Yosia, Mwenyezi Mungu aliniambia, “Je, umeona yale Israeli asiye mwaminifu ameyatenda? Amepanda juu ya kila kilima kirefu, na chini ya kila mti uliotanda, na amefanya uzinzi huko.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena, Bwana akaniambia siku za mfalme Yosia, Je! Umeyaona aliyotenda Israeli mwenye kuasi? Amepanda juu ya kila mlima mrefu, akafanya huko mambo ya ukahaba, tena, chini ya kila mti wenye majani mabichi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati wa utawala wa mfalme Yosia, Mwenyezi-Mungu aliniambia hivi: “Je, umeona jinsi Israeli asiye mwaminifu alivyofanya? Aliniacha, akapanda juu ya kila kilima kirefu na kwenda chini ya kila mti wenye majani mabichi, akafanya ukahaba wake humo!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati wa utawala wa Mfalme Yosia, BWANA aliniambia, “Umeona kile ambacho Israeli asiyemwaminifu alichofanya? Amepanda juu ya kila kilima kirefu na chini ya kila mti uliotanda na amefanya uzinzi huko.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati wa utawala wa Mfalme Yosia, bwana aliniambia, “Umeona kile Israeli asiye mwaminifu amekifanya? Amepanda juu ya kila kilima kirefu, na chini ya kila mti uliotanda na amefanya uzinzi huko.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena, BWANA akaniambia siku za mfalme Yosia, Je! Umeyaona aliyotenda Israeli mwenye kuasi? Amepanda juu ya kila mlima mrefu, akafanya huko mambo ya ukahaba, tena, chini ya kila mti wenye majani mabichi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati wa utawala wa mfalme Yosia, Mwenyezi-Mungu aliniambia hivi: “Je, umeona jinsi Israeli asiye mwaminifu alivyofanya? Aliniacha, akapanda juu ya kila kilima kirefu na kwenda chini ya kila mti wenye majani mabichi, akafanya ukahaba wake humo!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana akaniambia siku za mfalme Yosia kwamba: Umeyaona, binti Isiraeli aliyoyafanya akiniacha? Alipanda kila kilima kirefu, akakaa chini ya kila mti wenye majani mengi kufanya ugoni palepale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena, BWANA akaniambia siku za mfalme Yosia, Je! Umeyaona aliyotenda Israeli mwenye kuasi? Amepanda juu ya kila mlima mrefu, akafanya huko mambo ya ukahaba, tena, chini ya kila mti wenye majani mabichi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika siku ya utawala wa mufalme Yosia, Yawe aliniambia hivi: Umeona jinsi yule Israeli asiyekuwa mwaminifu alivyofanya? Aliniacha, akapanda juu ya kila kilima kirefu na kwenda chini ya kila muti wenye majani mabichi, akafanya ukahaba wake kule!