Jeremiah 30:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Usiogope ee Yakobo mtumishi wangu, wala usifadhaike, ee Israeli; maana nitakuokoa huko mbali uliko, na wazawa wako kutoka uhamishoni. Utarudi na kuishi kwa amani, wala hakuna mtu atakayekuogopesha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Hivyo usiogope, ee Yakobo mtumishi wangu, usifadhaike, ee Israeli,’ asema Mwenyezi Mungu. ‘Hakika, nitakuokoa kutoka mbali, wazao wako kutoka nchi ya uhamisho wao. Yakobo atakuwa tena na amani na usalama, wala hakuna atakayemtia hofu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu hiyo usiogope, Ee Yakobo, mtumishi wangu, asema Bwana; wala usifadhaike, Ee Israeli; kwa maana, tazama, nitakuokoa toka mbali, na wazao wako toka nchi ya uhamisho wao; na Yakobo atarudi, naye atatulia na kustarehe, wala hapana mtu atakayemtia hofu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Usiogope ee Yakobo mtumishi wangu, wala usifadhaike, ee Israeli; maana nitakuokoa huko mbali uliko, na wazawa wako kutoka uhamishoni. Utarudi na kuishi kwa amani, wala hakuna mtu atakayekuogopesha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Hivyo usiogope, Ee Yakobo mtumishi wangu, usifadhaike, Ee Israeli,’ asema BWANA. ‘Hakika, nitakuokoa wewe kutoka mahali pa mbali, wazao wako kutoka nchi ya uhamisho wao, Yakobo atakuwa tena na amani na usalama, wala hakuna atakayemtia hofu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Hivyo usiogope, ee Yakobo mtumishi wangu, usifadhaike, ee Israeli,’ asema bwana. ‘Hakika, nitakuokoa kutoka mbali, wazao wako kutoka nchi ya uhamisho wao. Yakobo atakuwa tena na amani na usalama, wala hakuna atakayemtia hofu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa sababu hiyo usiogope, Ee Yakobo, mtumishi wangu, asema BWANA; wala usifadhaike, Ee Israeli; kwa maana, tazama, nitakuokoa toka mbali, na wazao wako toka nchi ya uhamisho wao; na Yakobo atarudi, naye atatulia na kustarehe, wala hapana mtu atakayemtia hofu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Usiogope ee Yakobo mtumishi wangu, wala usifadhaike, ee Israeli; maana nitakuokoa huko mbali uliko, na wazawa wako kutoka uhamishoni. Utarudi na kuishi kwa amani, wala hakuna mtu atakayekuogopesha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, asemavyo Bwana: Nawe, mtumishi wangu Yakobo, usiogope, wala usistuke, Isiraeli! Kwani utaniona, nikikuokoa na kukutoa katika nchi za mbali, nacho kizazi chako nitakitoa katika nchi, walikofungiwa. Yakobo atarudi, atatulia pasipo kusumbuliwa, kwani hakuna atakayemhangaisha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu hiyo usiogope, Ee Yakobo, mtumishi wangu, asema BWANA; wala usifadhaike, Ee Israeli; kwa maana, tazama, nitakuokoa toka mbali, na wazao wako toka nchi ya uhamisho wao; na Yakobo atarudi, naye atatulia na kustarehe, wala hapana mtu atakayemtia hofu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Usiogope ee Yakobo, mutumishi wangu, wala usifazaike, ee Israeli. –Ni ujumbe wa Yawe.– Maana nitakuokoa toka huko mbali unapokuwa, nitawaokoa wazao wako kutoka katika uhamisho. Utarudi na kuishi kwa amani, wala hakuna mutu atakayekuogopesha.