Jeremiah 30:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wapenzi wako wote wamekusahau; hawajali chochote juu yako, nimekupiga pigo la adui; umeadhibiwa bila huruma, kwa kuwa kosa lako ni kubwa, dhambi zako ni nyingi mno.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale walioungana nawe wote wamekusahau, hawajali chochote kukuhusu wewe. Nimekupiga vile adui angekupiga, na kukuadhibu vile mtu mkatili angekuadhibu, kwa sababu hatia yako ni kubwa mno, na dhambi zako ni nyingi sana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wote wakupendao wamekusahau; hawakutafuti; maana nimekujeruhi kwa jeraha ya adui, kwa adhabu ya mtu mkatili; kwa sababu ya ukubwa wa uovu wako, kwa sababu dhambi zako zilikuwa zimeongezeka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wapenzi wako wote wamekusahau; hawajali chochote juu yako, nimekupiga pigo la adui; umeadhibiwa bila huruma, kwa kuwa kosa lako ni kubwa, dhambi zako ni nyingi mno.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wale walioungana nawe wote wamekusahau, hawajali cho chote kukuhusu wewe. Nimekupiga kama vile ambavyo adui angelifanya na kukuadhibu kama vile ambavyo mtu mkatili angelifanya, kwa sababu hatia yako ni kubwa mno na dhambi zako ni nyingi sana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wale walioungana nawe wote wamekusahau, hawajali chochote kukuhusu wewe. Nimekupiga kama vile adui angelifanya, na kukuadhibu kama vile mtu mkatili angelifanya, kwa sababu hatia yako ni kubwa mno na dhambi zako ni nyingi sana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wote wakupendao wamekusahau; hawakutafuti; maana nimekujeruhi kwa jeraha la adui, kwa adhabu ya mtu mkatili; kwa sababu ya ukubwa wa uovu wako, kwa sababu dhambi zako zilikuwa zimeongezeka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wapenzi wako wote wamekusahau; hawajali chochote juu yako, nimekupiga pigo la adui; umeadhibiwa bila huruma, kwa kuwa kosa lako ni kubwa, dhambi zako ni nyingi mno.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wote waliokupenda wamekusahau, hawakuulizi tena, kwani nimekupiga, kama ninavyopiga mchukivu, nimekuchapa pasipo huruma, kwa kuwa ulifanya maovu mengi, kweli makosa yako ni makali.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wote wakupendao wamekusahau; hawakutafuti; maana nimekujeruhi kwa jeraha ya adui, kwa adhabu ya mtu mkatili; kwa sababu ya ukubwa wa uovu wako, kwa sababu dhambi zako zilikuwa zimeongezeka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wapenzi wako wote wamekusahau; hawajali kitu chochote juu yako. Nimekupiga sawa vile ungekuwa adui yangu. Umeazibiwa bila huruma, kwa sababu kosa lako ni kubwa, zambi zako ni nyingi sana.