Jeremiah 30:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Nitakurudishia afya yako, na madonda yako nitayaponya, japo wamekuita ‘Aliyetupwa’, ‘Mji Siyoni usio na wa kuutunza!’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini nitakurudishia afya yako na kuyaponya majeraha yako,’ asema Mwenyezi Mungu, ‘kwa sababu umeitwa mwenye kutupwa, Sayuni ambaye hakuna yeyote anayekujali.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema Bwana, kwa sababu wamekuita, mwenye kutupwa, wakisema, Ni Sayuni, ambao hapana mtu autakaye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Nitakurudishia afya yako, na madonda yako nitayaponya, japo wamekuita ‘Aliyetupwa’, ‘Mji Siyoni usio na wa kuutunza!’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini nitakurudishia afya yako na kuyaponya majeraha yako,’ asema BWANA, ‘kwa sababu umeitwa mwenye kutupwa, Sayuni ambaye hakuna ye yote anayekujali.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini nitakurudishia afya yako na kuyaponya majeraha yako,’ asema bwana, ‘kwa sababu umeitwa mwenye kutupwa, Sayuni ambaye hakuna yeyote anayekujali.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya majeraha yako, asema BWANA, kwa sababu wamekuita, mwenye kutupwa, wakisema, Ni Sayuni, mji ambao hakuna mtu autakaye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Nitakurudishia afya yako, na madonda yako nitayaponya, japo wamekuita ‘Aliyetupwa’, ‘Mji Siyoni usio na wa kuutunza!’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani ndivyo, asemavyo Bwana: Nitakupatia uzima tena, hata vidonda vyako nitaviponya, kwa kuwa wewe Sioni wamekuita Mfukuzwa kwa kwamba: Hakuna anayemwuliza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema BWANA, kwa sababu wamekuita, mwenye kutupwa, wakisema, Ni Sayuni, ambao hapana mtu autakaye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sasa wanakuita wewe Sayuni: “Aliyetupiliwa”, “Muji usioshugulikiwa na mutu”. Lakini nitakurudishia afya yako, nitaponyesha vidonda vyako. –Ni ujumbe wa Yawe.