Jeremiah 30:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Nitazirudisha tena fanaka za maskani ya Yakobo, na kuyaonea huruma makao yake; mji utajengwa upya juu ya magofu yake, na ikulu ya mfalme itasimama pale ilipokuwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “ ‘Nitarudisha baraka za mahema ya Yakobo, na kuhurumia maskani zake. Mji utajengwa tena juu ya magofu yake, nalo jumba la kifalme litasimama mahali pake halisi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana asema hivi, Tazama, nitarudisha tena hema za Yakobo zilizohamishwa, na kuyahurumia makao yake; nao mji huo utajengwa juu ya magofu yake wenyewe, nalo jumba litakaliwa, kama ilivyokuwa desturi yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Nitazirudisha tena fanaka za maskani ya Yakobo, na kuyaonea huruma makao yake; mji utajengwa upya juu ya magofu yake, na ikulu ya mfalme itasimama pale ilipokuwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Hili ndilo asemalo BWANA: “ ‘Nitarudisha baraka za mahema ya Yakobo na kuhurumia maskani yake. Mji utajengwa tena juu ya magofu yake, nalo jumba la kifalme litasimama mahali pake halisi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Hili ndilo asemalo bwana: “ ‘Nitarudisha baraka za mahema ya Yakobo, na kuhurumia maskani yake. Mji utajengwa tena juu ya magofu yake, nalo jumba la kifalme litasimama mahali pake halisi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA asema hivi, Tazama, nitarudisha tena hema za Yakobo zilizohamishwa, na kuyahurumia makao yake; nao mji huo utajengwa juu ya magofu yake wenyewe, nalo jumba litakaliwa, kama ilivyokuwa desturi yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Nitazirudisha tena fanaka za maskani ya Yakobo, na kuyaonea huruma makao yake; mji utajengwa upya juu ya magofu yake, na ikulu ya mfalme itasimama pale ilipokuwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Mtaniona, nikiyafungua mafungo ya mahema yake Yakobo, nikiyahurumia makao yake; nao mji utajengwa tena juu ya chungu zake, hata jumba kuu litakaa, kama yalipasavyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA asema hivi, Tazama, nitarudisha tena hema za Yakobo zilizohamishwa, na kuyahurumia makao yake; nao mji huo utajengwa juu ya magofu yake wenyewe, nalo jumba litakaliwa, kama ilivyokuwa desturi yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe anasema hivi: Nitatengeneza upya maisha ya jamaa za wazao wa Yakobo, nitayaonea makao yao huruma; muji wao utajengwa upya kwenye mabomoko yake, nyumba ya kifalme itasimama pahali ilipokuwa mbele.