Jeremiah 30:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Jiulizeni sasa na kufahamu: Je, mwanamume aweza kujifungua mtoto? Mbona basi, namwona kila mwanamume amejishika kiunoni kama mwanamke mwenye utungu na nyuso zao zimegeuka rangi?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ulizeni na mkaone: Je, mwanaume aweza kuzaa watoto? Kwa nini basi ninaona kila mwanaume mwenye nguvu ameweka mikono yake tumboni kama mwanamke aliye na uchungu wa kuzaa, kila uso ukigeuka rangi kabisa?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ulizeni sasa, mkaone kwamba mwanamume aona utungu wa uzazi; mbona, basi, ninaona kila mtu anaweka mikono yake viunoni, kama mwanamke aliye na utungu, na nyuso zote zimegeuka rangi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Jiulizeni sasa na kufahamu: Je, mwanamume aweza kujifungua mtoto? Mbona basi, namwona kila mwanamume amejishika kiunoni kama mwanamke mwenye utungu na nyuso zao zimegeuka rangi?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ulizeni na mkaone: Je, mwanaume aweza kuzaa watoto? Kwa nini basi ninaona kila mwanaume mwenye nguvu ameweka mikono yake tumboni kama mwanamke aliye na utungu wa kuzaa, kila uso umegeuka rangi kabisa?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ulizeni na mkaone: Je, mwanaume aweza kuzaa watoto? Kwa nini basi ninaona kila mwanaume mwenye nguvu ameweka mikono yake tumboni kama mwanamke aliye na utungu wa kuzaa, kila uso ukigeuka rangi kabisa?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ulizeni sasa, mkaone kwamba mwanamume aona uchungu wa uzazi; mbona, basi, ninaona kila mtu anaweka mikono yake viunoni, kama mwanamke aliye na uchungu, na nyuso zote zimegeuka rangi?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Jiulizeni sasa na kufahamu: Je, mwanamume aweza kujifungua mtoto? Mbona basi, namwona kila mwanamume amejishika kiunoni kama mwanamke mwenye utungu na nyuso zao zimegeuka rangi?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ulizeni, mwone, kama yuko mwanamume atakayezaa! Mbona nimewaona waume wote wakitia mikono yao viunoni pao kama mwanamke anayetaka kuzaa? Mbona nyuso zote zimegeuka, zikachujuka?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ulizeni sasa, mkaone kwamba mwanamume aona utungu wa uzazi; mbona, basi, ninaona kila mtu anaweka mikono yake viunoni, kama mwanamke aliye na utungu, na nyuso zote zimegeuka rangi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mujiulize sasa na kufahamu: Mwanaume anaweza kuzaa mutoto? Mbona basi, ninamwona kila mwanaume anajikamata kwenye kiuno kama mwanamuke anayesikia maumivu ya kuzaa na nyuso zimebadilika?