Jeremiah 31:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watakuja na kuimba kwa sauti juu ya mlima Siyoni, wataona fahari juu ya wema wangu mimi Mwenyezi-Mungu, kwa nafaka, divai na mafuta niwapavyo, kwa kondoo na ng'ombe kadhalika; maisha yao yatakuwa kama bustani iliyotiliwa maji, wala hawatadhoofika tena.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watakuja na kupiga kelele kwa furaha katika miinuko ya Sayuni; watashangilia ukarimu wa Mwenyezi Mungu: nafaka, divai mpya na mafuta, wana-kondoo wachanga na ndama wa makundi ya ng’ombe nitakaowapa. Watakuwa kama bustani iliyoneshewa vizuri, wala hawatahuzunika tena.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao watakuja, na kuimba katika mlima Sayuni, wataukimbilia wema wa Bwana, nafaka, na divai, na mafuta, na wachanga wa kondoo na wa ng'ombe; na roho zao zitakuwa kama bustani iliyotiwa maji; wala hawatahuzunika tena kabisa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watakuja na kuimba kwa sauti juu ya mlima Siyoni, wataona fahari juu ya wema wangu mimi Mwenyezi-Mungu, kwa nafaka, divai na mafuta niwapavyo, kwa kondoo na ng'ombe kadhalika; maisha yao yatakuwa kama bustani iliyotiliwa maji, wala hawatadhoofika tena.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watakuja na kupiga kelele kwa furaha katika miinuko ya Sayuni; watashangilia ukarimu wa BWANA: nafaka, divai mpya na mafuta, wana-kondoo wachanga na ndama wa makundi ya ng'ombe nitakaowapa. Watakuwa kama bustani iliyonyeshewa vizuri, wala hawatahuzunika tena.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watakuja na kupiga kelele kwa furaha katika miinuko ya Sayuni; watashangilia ukarimu wa bwana: nafaka, divai mpya na mafuta, wana-kondoo wachanga na ndama wa makundi ya ng’ombe nitakaowapa. Watakuwa kama bustani iliyonyeshewa vizuri, wala hawatahuzunika tena.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao watakuja, na kuimba katika mlima Sayuni, wataukimbilia wema wa BWANA, nafaka, na divai, na mafuta, na wachanga wa kondoo na wa ng'ombe; na roho zao zitakuwa kama bustani iliyotiwa maji; wala hawatahuzunika tena kabisa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watakuja na kuimba kwa sauti juu ya mlima Siyoni, wataona fahari juu ya wema wangu mimi Mwenyezi-Mungu, kwa nafaka, divai na mafuta niwapavyo, kwa kondoo na ng'ombe kadhalika; maisha yao yatakuwa kama bustani iliyotiliwa maji, wala hawatadhoofika tena.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watakuja, wapige vigelegele mlimani kwa Sioni na kuyakimbilia mema ya Bwana, ngano na mvinyo na mafuta na wana wa kondoo na ndama; ndipo, roho zao zitakapokuwa kama shamba lenye maji, hawatazimia tena kwa njaa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao watakuja, na kuimba katika mlima Sayuni, wataukimbilia wema wa BWANA, nafaka, na divai, na mafuta, na wachanga wa kondoo na wa ng’ombe; na roho zao zitakuwa kama bustani iliyotiwa maji; wala hawatahuzunika tena kabisa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watakuja na kuimba kwa sauti juu ya mulima Sayuni, watapata utukufu juu ya wema wangu mimi Yawe, kwa ajili ya ngano, divai na mafuta ninavyowapa, kwa ajili ya kondoo na ngombe vilevile; maisha yao yatakuwa kama bustani iliyotiliwa maji, wala hawataregea tena.