Jeremiah 31:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sasa, acha kulia, futa machozi yako, kwani utapata tuzo kwa kazi yako, mimi Mwenyezi-Mungu nimesema; watoto wenu watarudi kutoka nchi ya maadui zenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Izuie sauti yako kulia, na macho yako yasitoe machozi, kwa kuwa kazi yako itapata thawabu,” asema Mwenyezi Mungu. “Watarudi kutoka nchi ya adui.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana asema hivi, Zuia sauti yako, usilie, na macho yako yasitoke machozi; Maana kazi yako itapata thawabu, nao watakuja tena toka nchi ya adui; Ndivyo asemavyo Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sasa, acha kulia, futa machozi yako, kwani utapata tuzo kwa kazi yako, mimi Mwenyezi-Mungu nimesema; watoto wenu watarudi kutoka nchi ya maadui zenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hili ndilo asemalo BWANA: “Izuie sauti yako kulia na macho yako yasitoe machozi, kwa kuwa kazi yako itapata thawabu,” asema BWANA. “Watarudi kutoka nchi ya adui.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hili ndilo asemalo bwana: “Izuie sauti yako kulia, na macho yako yasitoe machozi, kwa kuwa kazi yako itapata thawabu,” asema bwana. “Watarudi kutoka nchi ya adui.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA asema hivi, Zuia sauti yako, usilie, na macho yako yasitoke machozi; Maana kazi yako itapata thawabu, nao watakuja tena toka nchi ya adui; Ndivyo asemavyo BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sasa, acha kulia, futa machozi yako, kwani utapata tuzo kwa kazi yako, mimi Mwenyezi-Mungu nimesema; watoto wenu watarudi kutoka nchi ya maadui zenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Ukataze umio wako, usilie! Nayo macho yako yakataze, yasitoe machozi! Kwani mshahara wa matendo yako uko, hao watarudi wakitoka katika nchi ya adui; ndivyo, asemavyo Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA asema hivi, Zuia sauti yako, usilie, na macho yako yasitoke machozi; Maana kazi yako itapata thawabu, nao watakuja tena toka nchi ya adui; Ndivyo asemavyo BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe anasema hivi: Acha kulia, panguza machozi yako, maana utapata malipo kwa kazi yako. –Ni ujumbe wa Yawe.– Watoto wenu watarudi kutoka inchi ya waadui zenu.