Jeremiah 31:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Efraimu ni mwanangu mpendwa; yeye ni mtoto wangu nimpendaye sana. Ndio maana kila ninapomtisha, bado naendelea kumkumbuka. Moyo wangu wamwelekea kwa wema; hakika nitamhurumia. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, Efraimu si mwanangu mpendwa, mtoto ninayependezwa naye? Ingawa mara kwa mara ninanena dhidi yake, bado ninamkumbuka. Kwa hiyo moyo wangu unamwonea shauku, nina huruma kubwa kwa ajili yake,” asema Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Je! Efraimu siye mwanangu mpendwa? Je! Siye mtoto apendezaye? Maana kila nisemapo neno juu yake, ningali nikimkumbuka sana; kwa sababu hiyo moyo wangu unataabika kwa ajili yake; bila shaka nitamrehemu, asema Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Efraimu ni mwanangu mpendwa; yeye ni mtoto wangu nimpendaye sana. Ndio maana kila ninapomtisha, bado naendelea kumkumbuka. Moyo wangu wamwelekea kwa wema; hakika nitamhurumia. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, Efraimu si mwanangu mpendwa, mtoto ninayependezwa naye? Ingawa mara kwa mara ninanena dhidi yake, bado ninamkumbuka. Kwa hiyo moyo wangu unamwonea shauku, nina huruma kubwa kwa ajili yake,” asema BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, Efraimu si mwanangu mpendwa, mtoto ninayependezwa naye? Ingawa mara kwa mara ninanena dhidi yake, bado ninamkumbuka. Kwa hiyo moyo wangu unamwonea shauku, nina huruma kubwa kwa ajili yake,” asema bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Je! Efraimu siye mwanangu mpendwa? Je! Siye mtoto apendezaye? Maana kila nisemapo neno juu yake, ningali nikimkumbuka sana; kwa sababu hiyo moyo wangu unataabika kwa ajili yake; bila shaka nitamrehemu, asema BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Efraimu ni mwanangu mpendwa; yeye ni mtoto wangu nimpendaye sana. Ndio maana kila ninapomtisha, bado naendelea kumkumbuka. Moyo wangu wamwelekea kwa wema; hakika nitamhurumia. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Je? Efuraimu siye mwanangu mwenye kiasi kikuu? Siye mtoto wa kupendezwa naye? Ijapo nimemtisha, ninamkumbuka tena, nao moyo wangu unajihangaisha kwa ajili yake, mpaka nimhurumie; ndivyo, asemavyo Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Je! Efraimu siye mwanangu mpendwa? Je! Siye mtoto apendezaye? Maana kila nisemapo neno juu yake, ningali nikimkumbuka sana; kwa sababu hiyo moyo wangu unataabika kwa ajili yake; bila shaka nitamrehemu, asema BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Efuraimu ni mwana wangu mupendwa; yeye ni mutoto wangu ninayemupenda sana. Ndiyo maana kila mara ninapomutisha, ninaendelea kumukumbuka. Moyo wangu unamwelekea kwa wema; hakika nitamuhurumia. –Ni ujumbe wa Yawe.