Jeremiah 31:29 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku hizo watu hawatasema tena: ‘Wazee walikula zabibu chungu, na meno ya watoto yakatiwa ganzi.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Katika siku hizo, watu hawatasema tena, “ ‘Baba wamekula zabibu chachu, nayo meno ya watoto yakatiwa ganzi.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Siku zile, hawatasema tena, Baba za watu wamekula zabibu kali, na meno ya watoto wao yametiwa ganzi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku hizo watu hawatasema tena: ‘Wazee walikula zabibu chungu, na meno ya watoto yakatiwa ganzi.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Katika siku hizo watu hawatasema tena, “ ‘Baba wamekula zabibu chachu, nayo meno ya watoto yakatiwa ganzi.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Katika siku hizo, watu hawatasema tena, “ ‘Baba wamekula zabibu chachu, nayo meno ya watoto yakatiwa ganzi.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Siku zile, hawatasema tena, Baba za watu wamekula zabibu kali, na meno ya watoto wao yametiwa ganzi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku hizo watu hawatasema tena: ‘Wazee walikula zabibu chungu, na meno ya watoto yakatiwa ganzi.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku zile hawatasema tena: Baba walipokula zabibu bichi, ndipo, wana walipokufa ganzi la meno.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Siku zile, hawatasema tena, Baba za watu wamekula zabibu kali, na meno ya watoto wao yametiwa ganzi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku hizo watu hawatasema tena: Wazee walikula matunda mabichi ya mizabibu, na meno ya watoto ndiyo yanaumizwa.