Jeremiah 31:34 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wala haitawabidi kufundishana na kusema: ‘Mjue Mwenyezi-Mungu’, kwa sababu wote, wadogo kwa wakubwa, watanijua mimi Mungu. Maana nitawasamehe makosa yao, wala sitazikumbuka tena dhambi zao.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtu hatamfundisha tena jirani yake, wala mtu kumfundisha ndugu yake, akisema, ‘Mjue Mwenyezi Mungu,’ kwa sababu wote watanijua mimi, kuanzia aliye mdogo hata aliye mkubwa kuliko wote,” asema Mwenyezi Mungu. “Nitasamehe uovu wao, wala sitazikumbuka dhambi zao tena.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wala haitawabidi kufundishana na kusema: ‘Mjue Mwenyezi-Mungu’, kwa sababu wote, wadogo kwa wakubwa, watanijua mimi Mungu. Maana nitawasamehe makosa yao, wala sitazikumbuka tena dhambi zao.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mtu hatamfundisha tena jirani yake, au mtu kumfundisha ndugu yake akisema, ‘Umjue BWANA Mungu,’ kwa sababu wote watanijua mimi, kuanzia aliye mdogo kabisa kwao hata aliye mkuu sana,” asema BWANA. “Kwa sababu nitausamehe uovu wao na sitazikumbuka dhambi zao tena.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mtu hatamfundisha tena jirani yake, wala mtu kumfundisha ndugu yake akisema, ‘Mjue bwana Mwenyezi Mungu,’ kwa sababu wote watanijua mimi, tangu aliye mdogo kabisa kwao, hadi aliye mkuu sana,” asema bwana. “Kwa sababu nitasamehe uovu wao, wala sitazikumbuka dhambi zao tena.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue BWANA; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hadi aliye mkubwa miongoni mwao, asema BWANA; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wala haitawabidi kufundishana na kusema: ‘Mjue Mwenyezi-Mungu’, kwa sababu wote, wadogo kwa wakubwa, watanijua mimi Mungu. Maana nitawasamehe makosa yao, wala sitazikumbuka tena dhambi zao.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hawatafundishana tena mtu na mwenziwe, wala mtu na ndugu yake kwamba: Mjueni Bwana! Kwani wote watanijua, hivyo walivyo wadogo, mpaka wakiwa wakubwa, kwani nitawaondolea manza zao, walizozikora, nisiyakumbuke tena makosa yao; ndivyo, asemavyo Bwana.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue BWANA; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema BWANA; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wala hawatafundishana tena kila mutu na jirani yake, na kila mutu na ndugu yake na kusema “Mumujue Yawe”, kwa sababu wote, wadogo kama vile wakubwa, watanijua mimi Mungu. Maana nitawasamehe makosa yao, wala sitazikumbuka tena zambi zao.