Jeremiah 31:36 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Mimi hulifanya jua liangaze mchana, mwezi na nyota vimulike usiku; pia mimi huitikisa bahari, nayo hutoa mawimbi. Jina langu mimi ni Mwenyezi-Mungu wa majeshi. Basi, nami nasema: Kadiri ninavyotegemeza mipango hiyo yote yangu kadiri hiyohiyo Israeli watakavyobaki kuwa watu wangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ikiwa amri hizi zitaondoka machoni pangu,” asema Mwenyezi Mungu, “ndipo wazao wa Israeli watakoma kuwa taifa mbele yangu daima.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Amri hizi zikiondoka, zisiwe mbele zangu, asema Bwana, ndipo wazao wa Israeli nao wataacha kuwa taifa mbele zangu milele.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Mimi hulifanya jua liangaze mchana, mwezi na nyota vimulike usiku; pia mimi huitikisa bahari, nayo hutoa mawimbi. Jina langu mimi ni Mwenyezi-Mungu wa majeshi. Basi, nami nasema: Kadiri ninavyotegemeza mipango hiyo yote yangu kadiri hiyohiyo Israeli watakavyobaki kuwa watu wangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ikiwa amri hizi zitaondoka machoni pangu,” asema BWANA, “ndipo wazao wa Israeli watakoma kuwa taifa mbele yangu daima.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ikiwa amri hizi zitaondoka machoni pangu,” asema bwana, “ndipo wazao wa Israeli watakoma kuwa taifa mbele yangu daima.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Amri hizi zikiondoka, zisiwe mbele zangu, asema BWANA, ndipo wazao wa Israeli nao wataacha kuwa taifa mbele zangu milele.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Mimi hulifanya jua liangaze mchana, mwezi na nyota vimulike usiku; pia mimi huitikisa bahari, nayo hutoa mawimbi. Jina langu mimi ni Mwenyezi-Mungu wa majeshi. Basi, nami nasema: Kadiri ninavyotegemeza mipango hiyo yote yangu kadiri hiyohiyo Israeli watakavyobaki kuwa watu wangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
basi, ndivyo, asemavyo Bwana: Hapo, matengenezo hayo yatakapotoweka machoni pangu, ndipo, walio wa kizazi cha Isiraeli watakapokoma, wasiwe taifa la siku zote machoni pangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Amri hizi zikiondoka, zisiwe mbele zangu, asema BWANA, ndipo wazao wa Israeli nao wataacha kuwa taifa mbele zangu milele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ikiwa itanifikia kuvunja mipango ile, halafu nitaweza vilevile kukomesha kizazi cha Waisraeli, wasiitwe tena taifa langu siku zote. –Ni ujumbe wa Yawe.