Jeremiah 31:40 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Bonde lote walimozikwa wafu na kutupiwa majivu, mashamba yote, mpaka kijito cha Kidroni, mpaka pembe ya lango la Farasi kuelekea mashariki, litakuwa eneo takatifu kwa Mwenyezi-Mungu. Hakuna kitakachoharibiwa humo wala kubomolewa tena milele.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
wanakotupa maiti na majivu, na maeneo yote kuanzia Bonde la Kidroni upande wa mashariki hadi pembe ya Lango la Farasi patakuwa mahali patakatifu kwa Mwenyezi Mungu. Mji huu kamwe hautang’olewa wala kubomolewa tena.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na bonde lote la mizoga, na majivu, na mashamba yote mpaka kijito Kidroni, mpaka pembe ya lango la farasi, upande wa mashariki, patakuwa patakatifu kwa Bwana; hapatang'olewa, wala hapatabomolewa, hata milele.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Bonde lote walimozikwa wafu na kutupiwa majivu, mashamba yote, mpaka kijito cha Kidroni, mpaka pembe ya lango la Farasi kuelekea mashariki, litakuwa eneo takatifu kwa Mwenyezi-Mungu. Hakuna kitakachoharibiwa humo wala kubomolewa tena milele.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Bonde lote watupwapo maiti na majivu pia na matuta yote kutoka Bonde la Kidroni upande wa mashariki mpaka kwenye pembe ya Lango la Farasi, itakuwa takatifu kwa BWANA. Kamwe mji huu hautang'olewa tena wala kubomolewa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Bonde lote watupwapo maiti na majivu pia na matuta yote kutoka Bonde la Kidroni upande wa mashariki hadi pembe ya Lango la Farasi, itakuwa takatifu kwa bwana. Kamwe mji huu hautang’olewa tena wala kubomolewa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na bonde lote la mizoga, na majivu, na mashamba yote mpaka kijito Kidroni, mpaka pembe ya lango la farasi, upande wa mashariki, patakuwa patakatifu kwa BWANA; hapatang'olewa, wala hapatabomolewa, hata milele.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Bonde lote walimozikwa wafu na kutupiwa majivu, mashamba yote, mpaka kijito cha Kidroni, mpaka pembe ya lango la Farasi kuelekea mashariki, litakuwa eneo takatifu kwa Mwenyezi-Mungu. Hakuna kitakachoharibiwa humo wala kubomolewa tena milele.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nalo bonde lote la mizoga na la majivu na mashamba yote mpaka kwenye mto wa Kidoroni na mpaka pembeni kwa Lango la Farasi lililoko upande wa maawioni kwa jua yatakuwa Patakatifu pa Bwana, hapatang'olewa tena, wala hapatavunjwa tena kale na kale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na bonde lote la mizoga, na majivu, na mashamba yote mpaka kijito Kidroni, mpaka pembe ya lango la farasi, upande wa mashariki, patakuwa patakatifu kwa BWANA; hapatang’olewa, wala hapatabomolewa, hata milele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Bonde lote walimozikwa wafu na kutupiwa majivu, mashamba yote, mpaka kijito cha Kidroni, mpaka pembe ya mulango wa Farasi kuelekea upande wa mashariki, litakuwa eneo takatifu kwa Yawe. Hakuna kitakachoharibiwa humo wala kubomolewa tena milele.