Jeremiah 31:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana siku yaja ambapo mlinzi atapiga mbiu katika vilima vya Efraimu: ‘Amkeni, twende juu mpaka Siyoni kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku inakuja ambapo walinzi watapiga kelele juu ya vilima vya Efraimu, wakisema, ‘Njooni, twendeni juu Sayuni, kwake Mwenyezi Mungu, Mungu wetu.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana kutakuwa siku moja, ambayo walinzi watalia juu ya vilima vya Efraimu, Inukeni, tukaende Sayuni, kwa Bwana, Mungu wetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana siku yaja ambapo mlinzi atapiga mbiu katika vilima vya Efraimu: ‘Amkeni, twende juu mpaka Siyoni kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Itakuja siku wakati walinzi watakapowapigia kelele juu ya vilima vya Efraimu wakisema, ‘Njoni, twendeni juu Sayuni, kwake BWANA Mungu wetu.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Itakuja siku wakati walinzi watakapowapigia kelele juu ya vilima vya Efraimu wakisema, ‘Njooni, twendeni juu Sayuni, kwake bwana Mwenyezi Mungu wetu.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana kutakuwa siku moja, ambayo walinzi watalia juu ya vilima vya Efraimu, Inukeni, tukaende Sayuni, kwa BWANA, Mungu wetu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana siku yaja ambapo mlinzi atapiga mbiu katika vilima vya Efraimu: ‘Amkeni, twende juu mpaka Siyoni kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani iko siku, walinzi watakapoita mlimani kwa Efuraimu kwamba: Inukeni, tupande kwenda Sioni kwa Bwana Mungu wetu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana kutakuwa siku moja, ambayo walinzi watalia juu ya vilima vya Efraimu, Inukeni, tukaende Sayuni, kwa BWANA, Mungu wetu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maana kutakuja siku ambapo walinzi watalalamika hivi katika vilima vya Efuraimu: Musimame, tupande kwenda Sayuni kwa Yawe, Mungu wetu.