Jeremiah 31:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tazama, nitawaleta kutoka nchi ya kaskazini, nitawakusanya kutoka miisho ya dunia. Wote watakuwapo hapo; hata vipofu na vilema, wanawake waja wazito na wanaojifungua; umati mkubwa sana utarudi hapa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tazama, nitawaleta kutoka nchi ya kaskazini na kuwakusanya kutoka miisho ya dunia. Miongoni mwao watakuwa vipofu na viwete, mama wajawazito na wenye uchungu wa kuzaa. Umati mkubwa wa watu watarudi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tazama, nitawaleta toka nchi ya kaskazini, na kuwakusanya katika miisho ya dunia, na pamoja nao watakuja walio vipofu, na hao wachechemeao, mwanamke mwenye mimba, na yeye pia aliye na utungu wa kuzaa; watarudi huko, jeshi kubwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tazama, nitawaleta kutoka nchi ya kaskazini, nitawakusanya kutoka miisho ya dunia. Wote watakuwapo hapo; hata vipofu na vilema, wanawake waja wazito na wanaojifungua; umati mkubwa sana utarudi hapa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tazama, nitawaleta kutoka nchi ya kaskazini na kuwakusanya kutoka miisho ya dunia. Miongoni mwao watakuwepo vipofu na viwete, mama wajawazito na wenye utungu wa kuzaa, umati mkubwa wa watu utarudi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tazama, nitawaleta kutoka nchi ya kaskazini na kuwakusanya kutoka miisho ya dunia. Miongoni mwao watakuwepo vipofu na viwete, mama wajawazito na wenye utungu wa kuzaa. Umati mkubwa wa watu utarudi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tazama, nitawaleta toka nchi ya kaskazini, na kuwakusanya katika miisho ya dunia, na pamoja nao watakuja walio vipofu, na hao wachechemeao, mwanamke mwenye mimba, na yeye pia aliye na uchungu wa kuzaa; watarudi huko, jeshi kubwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tazama, nitawaleta kutoka nchi ya kaskazini, nitawakusanya kutoka miisho ya dunia. Wote watakuwapo hapo; hata vipofu na vilema, wanawake waja wazito na wanaojifungua; umati mkubwa sana utarudi hapa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtaniona, nikiwaleta na kuwatoa katika nchi ya upande wa kaskazini, nikiwakusanya na kuwatoa mapeoni kwa nchi, nao vipofu na viwete, hata wenye mimba pamoja nao wazaao, watakuwa kundi kubwa, watakaporudi huku.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tazama, nitawaleta toka nchi ya kaskazini, na kuwakusanya katika miisho ya dunia, na pamoja nao watakuja walio vipofu, na hao wachechemeao, mwanamke mwenye mimba, na yeye pia aliye na utungu wa kuzaa; watarudi huko, jeshi kubwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitawarudisha kutoka inchi ya kaskazini, nitawakusanya kutoka miisho ya dunia. Wote watakuwa pale; hata vipofu na vilema, wanawake wenye mimba na wanaosikia maumivu ya kuzaa; kundi kubwa sana la watu litarudi hapa.