Jeremiah 31:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watarudi wakiwa wanatoa machozi, nitawarudisha nikiwafariji; nitawapitisha kando ya vijito vya maji, katika njia iliyonyoka ambamo hawatajikwaa; maana mimi nimekuwa baba wa Israeli, Efraimu ni mzaliwa wangu wa kwanza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watakuja wakilia; wataomba wakati ninawarudisha. Nitawaongoza kando ya vijito vya maji, katika njia iliyonyooka hawatajikwaa, kwa sababu mimi ndimi baba wa Israeli, naye Efraimu ni mzaliwa wangu wa kwanza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Watakuja kwa kulia, na kwa maombi nitawaongoza; nitawaendesha penye mito ya maji, katika njia iliyonyoka; katika njia hiyo hawatajikwaa; maana mimi ni baba wa Israeli, na Efraimu ni mzaliwa wa kwanza wangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watarudi wakiwa wanatoa machozi, nitawarudisha nikiwafariji; nitawapitisha kando ya vijito vya maji, katika njia iliyonyoka ambamo hawatajikwaa; maana mimi nimekuwa baba wa Israeli, Efraimu ni mzaliwa wangu wa kwanza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watakuja wakilia; wataomba wakati nikiwarudisha. Nitawaongoza kando ya vijito vya maji katika mapito yaliyo tambarare ambapo hawatajikwaa, kwa sababu mimi ndimi baba wa Israeli, naye Efraimu ni mwanangu, mzaliwa wangu wa kwanza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watakuja wakilia; wataomba wakati ninawarudisha. Nitawaongoza kando ya vijito vya maji katika mapito yaliyo tambarare ambapo hawatajikwaa, kwa sababu mimi ndimi baba wa Israeli, naye Efraimu ni mzaliwa wangu wa kwanza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Watakuja kwa kulia, na kwa maombi nitawaongoza; nitawapitisha kwenye mito ya maji, katika njia iliyonyoka; katika njia hiyo hawatajikwaa; maana mimi ni baba wa Israeli, na Efraimu ni mzaliwa wa kwanza wangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watarudi wakiwa wanatoa machozi, nitawarudisha nikiwafariji; nitawapitisha kando ya vijito vya maji, katika njia iliyonyoka ambamo hawatajikwaa; maana mimi nimekuwa baba wa Israeli, Efraimu ni mzaliwa wangu wa kwanza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watakuja na kulia, nami nitawaongoza, wakinilalamikia; nitawapeleka kwenye vijito vya maji na kushika njia inyokayo, wasijikwae hapo, kwani nitakuwa baba yao Waisiraeli, nao Waefuraimu watakuwa kama mwanangu wa kwanza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Watakuja kwa kulia, na kwa maombi nitawaongoza; nitawaendesha penye mito ya maji, katika njia iliyonyoka; katika njia hiyo hawatajikwaa; maana mimi ni baba wa Israeli, na Efraimu ni mzaliwa wa kwanza wangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watarudi wakiwa wanatoa machozi, nami nitawaongoza nikiwafariji; nitawapitisha kando ya vijito vya maji, katika njia iliyonyooka ambamo hawatajikwaa; maana mimi nimekuwa baba wa Israeli, Efuraimu ni muzaliwa wangu wa kwanza.