Jeremiah 32:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nilimpa hiyo hati ya ununuzi Baruku mwana wa Neria mwana wa Maaseya, mbele ya binamu yangu Hanameli na mashahidi waliokuwa wametia sahihi hati ya ununuzi, na mbele ya Wayahudi wote waliokuwa wameketi katika ukumbi wa walinzi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
nami nikampa Baruku mwana wa Neria, mwana wa Maaseya, hati hii mbele ya binamu yangu Hanameli, na mbele ya mashahidi waliokuwa wameweka sahihi kwenye hati hii na mbele ya Wayahudi wote waliokuwa wameketi katika ua wa walinzi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na ile hati ya kununua nikampa Baruku, mwana wa Neria, mwana wa Maaseya, mbele ya uso wa Hanameli, mwana wa mjomba wangu, na mbele ya mashahidi wale walioitia sahihi hati ya kununua, mbele ya Wayahudi wote walioketi katika uwanda wa walinzi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nilimpa hiyo hati ya ununuzi Baruku mwana wa Neria mwana wa Maaseya, mbele ya binamu yangu Hanameli na mashahidi waliokuwa wametia sahihi hati ya ununuzi, na mbele ya Wayahudi wote waliokuwa wameketi katika ukumbi wa walinzi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
nami nikampa Baruki mwana wa Neria, mwana wa Maaseya, hati hii mbele ya binamu yangu Hanameli na mbele ya mashahidi waliokuwa wameweka sahihi kwenye hati hii na mbele ya Wayahudi wote waliokuwa wameketi katika ua wa walinzi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
nami nikampa Baruku mwana wa Neria, mwana wa Maaseya, hati hii mbele ya binamu yangu Hanameli, na mbele ya mashahidi waliokuwa wameweka sahihi kwenye hati hii na mbele ya Wayahudi wote waliokuwa wameketi katika ua wa walinzi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na ile hati ya kununua nikampa Baruku, mwana wa Neria, mwana wa Maaseya, mbele ya uso wa Hanameli, mwana wa mjomba wangu, na mbele ya mashahidi wale walioitia sahihi hati ya kununua, mbele ya Wayahudi wote walioketi katika ukumbi wa walinzi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nilimpa hiyo hati ya ununuzi Baruku mwana wa Neria mwana wa Maaseya, mbele ya binamu yangu Hanameli na mashahidi waliokuwa wametia sahihi hati ya ununuzi, na mbele ya Wayahudi wote waliokuwa wameketi katika ukumbi wa walinzi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hicho cheti cha ununuzi nikampa Baruku, mwana wa Neria, mwana wa Masea, machoni pake Hanameli, mwana wa mjomba wangu, napo machoni pao mashahidi walioyaandika majina yao katika cheti cha ununuzi napo machoni pao Wayuda wote waliokaa uani penye kifungo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na ile hati ya kununua nikampa Baruku, mwana wa Neria, mwana wa Maaseya, mbele ya uso wa Hanameli, mwana wa mjomba wangu, na mbele ya mashahidi wale walioitia sahihi hati ya kununua, mbele ya Wayahudi wote walioketi katika uwanda wa walinzi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nilimupa Baruku mwana wa Neria mujukuu wa Masea ile barua ya ununuzi mbele ya binamu yangu Hanameli na washuhuda waliokuwa wametia sahihi juu ya barua ya ununuzi, na mbele ya Wayuda wote waliokuwa wameikaa katika baraza la walinzi.