Jeremiah 32:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wewe unaonesha fadhili zako kwa maelfu ya watu; lakini pia unawaadhibu watu kwa sababu ya dhambi za wazee wao. Wewe ni Mungu mkuu, mwenye nguvu, Mwenyezi-Mungu wa Majeshi ndilo jina lako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wewe huonesha upendo kwa maelfu, lakini huleta adhabu kwa ajili ya dhambi za baba mapajani mwa watoto wao baada yao. Ee Mungu mkuu na mwenye uweza, ambaye jina lako ni Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wewe uwarehemuye watu elfu nyingi, uwalipaye baba za watu uovu wao vifuani mwa watoto wao baada yao; Mungu aliye mkuu, aliye hodari, Bwana wa majeshi ndilo jina lake;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wewe unaonesha fadhili zako kwa maelfu ya watu; lakini pia unawaadhibu watu kwa sababu ya dhambi za wazee wao. Wewe ni Mungu mkuu, mwenye nguvu, Mwenyezi-Mungu wa Majeshi ndilo jina lako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huonyesha upendo kwa maelfu lakini huleta adhabu kwa ajili ya dhambi za baba mapajani mwa watoto wao baada yao. Ee Mungu mkuu na mwenye uweza, ambaye jina lako ni BWANA Mwenye Nguvu Zote,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wewe huonyesha upendo kwa maelfu, lakini huleta adhabu kwa ajili ya dhambi za baba mapajani mwa watoto wao baada yao. Ee Mungu mkuu na mwenye uweza, ambaye jina lako ni bwana Mwenye Nguvu Zote,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wewe uwarehemuye watu elfu nyingi, uwalipaye baba za watu uovu wao vifuani mwa watoto wao baada yao; Mungu aliye mkuu, aliye hodari, BWANA wa majeshi ndilo jina lake;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wewe unaonesha fadhili zako kwa maelfu ya watu; lakini pia unawaadhibu watu kwa sababu ya dhambi za wazee wao. Wewe ni Mungu mkuu, mwenye nguvu, Mwenyezi-Mungu wa Majeshi ndilo jina lako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watu maelfu huwahurumia, nazo manza, baba walizozikora, huzilipiza kwa wana wao waliotokea nyuma yao. U Mungu mkuu mwenye nguvu; Bwana Mwenye vikosi ni Jina lako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wewe uwarehemuye watu elfu nyingi, uwalipaye baba za watu uovu wao vifuani mwa watoto wao baada yao; Mungu aliye mkuu, aliye hodari, BWANA wa majeshi ndilo jina lake;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wewe unaonyesha mema yako kwa maelfu ya watu; lakini unawaazibu vilevile watu kwa sababu ya zambi za babu zao. Wewe ni Mungu Mukubwa, mwenye nguvu, Yawe wa majeshi ndilo jina lako.