Jeremiah 32:29 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakaldayo wanaoushambulia mji huu wataingia na kuuchoma moto; watauteketeza pamoja na nyumba ambazo juu ya paa zake ubani ulifukiziwa mungu Baali na tambiko za divai zilimiminiwa miungu mingine, ili kunichokoza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakaldayo ambao wanaushambulia mji huu watakuja na kuuchoma moto na kuuteketeza, pamoja na nyumba ambamo watu wamenikasirisha kwa kumfukizia Baali uvumba katika mapaa na kumimina sadaka za vinywaji kwa miungu mingine.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na Wakaldayo, wanaopigana na mji huu, watakuja, na kuutia moto mji huu, na kuuteketeza, pamoja na nyumba zake, ambazo juu ya dari zake wamemfukizia Baali uvumba, na kuwamiminia miungu mingine vinywaji, ili kunikasirisha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakaldayo wanaoushambulia mji huu wataingia na kuuchoma moto; watauteketeza pamoja na nyumba ambazo juu ya paa zake ubani ulifukiziwa mungu Baali na tambiko za divai zilimiminiwa miungu mingine, ili kunichokoza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakaldayo ambao wanaushambulia mji huu watakuja na kuuchoma moto na kuuteketeza, pamoja na nyumba ambamo ndani yake watu wamenikasirisha kwa kumfukizia Baali uvumba katika mapaa na kumimina sadaka ya kinywaji kwa miungu mingine.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakaldayo ambao wanaushambulia mji huu watakuja na kuuchoma moto na kuuteketeza, pamoja na nyumba ambamo watu wamenikasirisha kwa kumfukizia Baali uvumba katika mapaa na kumimina sadaka za vinywaji kwa miungu mingine.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na Wakaldayo, wanaopigana na mji huu, watakuja, na kuutia moto mji huu, na kuuteketeza, pamoja na nyumba zake, ambazo juu ya madari yake wamemfukizia Baali uvumba, na kuwamiminia miungu mingine vinywaji, ili kunikasirisha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakaldayo wanaoushambulia mji huu wataingia na kuuchoma moto; watauteketeza pamoja na nyumba ambazo juu ya paa zake ubani ulifukiziwa mungu Baali na tambiko za divai zilimiminiwa miungu mingine, ili kunichokoza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kweli Wakasidi wanaoupigia mji huu vita watauingia, watauchoma moto mji huu na kuziteketeza nyumba, walimomvukizia Baali darini juu, nazo zile, walimomwagia miungu mingine vinywaji vya tambiko, kusudi wanikasirishe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na Wakaldayo, wanaopigana na mji huu, watakuja, na kuutia moto mji huu, na kuuteketeza, pamoja na nyumba zake, ambazo juu ya dari zake wamemfukizia Baali uvumba, na kuwamiminia miungu mingine vinywaji, ili kunikasirisha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakaldea wanaoushambulia muji huu wataingia na kuuteketeza kwa moto; watauteketeza pamoja na nyumba ambazo juu ya paa zake ubani ulifukiziwa kwa mungu Bali na sadaka za divai zilitolewa kwa miungu mingine, kwa kunichokoza.