Jeremiah 32:35 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walimjengea mungu Baali madhabahu katika bonde la Mwana wa Hinomu, ili wamtolee mungu Moleki wavulana wao na binti zao, ingawa sikuwaamuru wala sikufikiria kwamba wangefanya hivyo, wakawafanya watu wa Yuda watende dhambi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakajenga mahali pa juu pa kuabudia Baali katika Bonde la Ben-Hinomu, ambapo waliwatoa kafara watoto wao wa kiume na wa kike kwa Moleki, ingawa kamwe sikuwaamuru, wala sikuwaza kwamba watafanya chukizo kama hilo na kumfanya Yuda atende dhambi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena walijenga mahali palipoinuka kwa Baali, palipo katika bonde la mwana wa Hinomu, ili kuwapitisha wana wao na binti zao katika moto kwa ajili ya Moleki, jambo nisilowaagiza; wala halikuingia moyoni mwangu kwamba walitende chukizo hilo; wapate kumkosesha Yuda.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walimjengea mungu Baali madhabahu katika bonde la Mwana wa Hinomu, ili wamtolee mungu Moleki wavulana wao na binti zao, ingawa sikuwaamuru wala sikufikiria kwamba wangefanya hivyo, wakawafanya watu wa Yuda watende dhambi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakajenga mahali pa juu pa kuabudia miungu kwa ajili ya Baali katika Bonde la Ben-Hinomu ambapo walitoa wana wao na binti zao kafara kwa Moleki, ingawa kamwe sikuamuru, wala halikuingia akilini mwangu, kwamba watafanya chukizo kama hilo na kumfanya Yuda atende dhambi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakajenga mahali pa juu pa kuabudia miungu kwa ajili ya Baali katika Bonde la Ben-Hinomu, ambapo walitoa wana wao na binti zao kafara kwa Moleki, ingawa kamwe sikuamuru, wala halikuingia akilini mwangu, kwamba watafanya chukizo kama hilo na kumfanya Yuda atende dhambi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena walijenga mahali palipoinuka kwa Baali, palipo katika bonde la mwana wa Hinomu, ili kuwapitisha wana wao na binti zao katika moto kwa ajili ya Moleki, jambo nisilowaagiza; wala halikuingia moyoni mwangu kwamba walitende chukizo hilo; wapate kumkosesha Yuda.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walimjengea mungu Baali madhabahu katika bonde la Mwana wa Hinomu, ili wamtolee mungu Moleki wavulana wao na binti zao, ingawa sikuwaamuru wala sikufikiria kwamba wangefanya hivyo, wakawafanya watu wa Yuda watende dhambi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakamjengea Baali pa kumtambikia vilimani juu katika Bonde la Mwana wa Hinomu, wawatumie wana wao wa kiume na wa kike kuwa ng'ombe za tambiko za Moloki, nami sikuwaagiza hivyo, wala havikunijia moyoni, ya kuwa watafanya tapisho kama hilo, kusudi wawakoseshe Wayuda.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena walijenga mahali palipoinuka kwa Baali, palipo katika bonde la mwana wa Hinomu, ili kuwapitisha wana wao na binti zao katika moto kwa ajili ya Moleki, jambo nisilowaagiza; wala halikuingia moyoni mwangu kwamba walitende chukizo hilo; wapate kumkosesha Yuda.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walimujengea mungu Bali mazabahu katika bonde la Mwana wa Hinomu, kusudi wamutolee mungu Moleki wana wao na wabinti zao, ingawa sikuwaamuru wala sikufikiria kwamba wangefanya hivyo. Wakasukuma watu wa Yuda watende zambi.