Jeremiah 32:37 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitawakusanya watu kutoka nchi zote ambako kwa hasira na ghadhabu na chuki yangu kubwa, niliwatawanya. Nitawarudisha tena mahali hapa, na kuwafanya wakae salama.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hakika nitawakusanya kutoka nchi zote nilizowafukuzia katika hasira yangu kali na ghadhabu yangu kuu, nitawarudisha mahali hapa na kuwaruhusu waishi salama.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tazama, nitawakusanya, na kuwatoa katika nchi zote nilikowafukuza, katika hasira yangu, na uchungu wangu, na ghadhabu yangu nyingi; nami nitawaleta tena hata mahali hapa, nami nitawakalisha salama salimini;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitawakusanya watu kutoka nchi zote ambako kwa hasira na ghadhabu na chuki yangu kubwa, niliwatawanya. Nitawarudisha tena mahali hapa, na kuwafanya wakae salama.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hakika nitawakusanya kutoka katika nchi zote nilizowafukuzia katika hasira yangu kali na ghadhabu yangu kuu, nitawarudisha mahali hapa na kuwaruhusu waishi kwa salama.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hakika nitawakusanya kutoka nchi zote nilizowafukuzia katika hasira yangu kali na ghadhabu yangu kuu, nitawarudisha mahali hapa na kuwaruhusu waishi kwa salama.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tazama, nitawakusanya, na kuwatoa katika nchi zote nilikowafukuza, katika hasira yangu, na uchungu wangu, na ghadhabu yangu nyingi; nami nitawaleta tena hadi mahali hapa, nami nitawakalisha salama salimini;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitawakusanya watu kutoka nchi zote ambako kwa hasira na ghadhabu na chuki yangu kubwa, niliwatawanya. Nitawarudisha tena mahali hapa, na kuwafanya wakae salama.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtaniona, nikiwakusanya na kuwatoa katika nchi zote, nilikowaendesha na kuwakimbiza kwa makali yangu yaliyowaka moto na kwa machafuko makuu, nitawarudisha mahali hapa na kuwapa kukaa salama.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tazama, nitawakusanya, na kuwatoa katika nchi zote nilikowafukuza, katika hasira yangu, na uchungu wangu, na ghadhabu yangu nyingi; nami nitawaleta tena hata mahali hapa, nami nitawakalisha salama salimini;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitawakusanya watu kutoka inchi zote ambako kwa hasira na kasirani na chuki yangu kubwa, niliwatawanya. Nitawarudisha tena hapa, na kuwafanya wakae salama.