Jeremiah 33:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
sauti za harusi na za furaha, sauti za waimbaji wakati wakileta tambiko za shukrani katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu: ‘Mshukuruni Mwenyezi-Mungu wa majeshi kwa kuwa Mwenyezi-Mungu ni mwema, kwa maana fadhili zake zadumu milele.’ Nitairudishia nchi hii fanaka yake ya awali. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
sauti za shangwe na furaha, sauti za bibi arusi na bwana arusi, na sauti za wale waletao sadaka za shukrani katika nyumba ya Mwenyezi Mungu, wakisema, “ ‘ “Mshukuruni Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, kwa maana Mwenyezi Mungu ni mwema; fadhili zake zadumu milele.” Kwa kuwa nitairudishia nchi baraka kama ilivyokuwa hapo awali,’ asema Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
itasikilikana tena sauti ya furaha na sauti ya shangwe, sauti ya bwana arusi na sauti ya bibi arusi, sauti yao wasemao Mshukuruni Bwana wa majeshi, maana Bwana ni mwema, rehema zake ni za milele; na sauti zao waletao sadaka za shukrani nyumbani kwa Bwana. Kwa kuwa nitawarudisha wafungwa wa nchi hii kama kwanza, asema Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
sauti za harusi na za furaha, sauti za waimbaji wakati wakileta tambiko za shukrani katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu: ‘Mshukuruni Mwenyezi-Mungu wa majeshi kwa kuwa Mwenyezi-Mungu ni mwema, kwa maana fadhili zake zadumu milele.’ Nitairudishia nchi hii fanaka yake ya awali. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
sauti za shangwe na furaha, sauti za bibi na bwana arusi na sauti za wale waletao sadaka za shukrani katika nyumba ya BWANA, wakisema, “ ‘ “Mshukuruni BWANA Mwenye Nguvu Zote, kwa maana BWANA ni mwema; upendo wake wadumu milele.” Kwa kuwa nitairudishia nchi baraka kama zilivyokuwa hapo awali,’ asema BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
sauti za shangwe na furaha, sauti za bibi na bwana arusi, na sauti za wale waletao sadaka za shukrani katika nyumba ya bwana, wakisema, “ ‘ “Mshukuruni bwana Mwenye Nguvu Zote, kwa maana bwana ni mwema; upendo wake wadumu milele.” Kwa kuwa nitairudishia nchi baraka kama zilivyokuwa hapo awali,’ asema bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
itasikika tena sauti ya furaha na sauti ya shangwe, sauti ya bwana harusi na sauti ya bibi harusi, sauti yao wasemao Mshukuruni BWANA wa majeshi, maana BWANA ni mwema, rehema zake ni za milele; na sauti zao waletao sadaka za shukrani nyumbani kwa BWANA. Kwa kuwa nitawarudisha wafungwa wa nchi hii kama kwanza, asema BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
sauti za harusi na za furaha, sauti za waimbaji wakati wakileta tambiko za shukrani katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu: ‘Mshukuruni Mwenyezi-Mungu wa majeshi kwa kuwa Mwenyezi-Mungu ni mwema, kwa maana fadhili zake zadumu milele.’ Nitairudishia nchi hii fanaka yake ya awali. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ndipo, patakaposikilika tena sauti za vicheko na sauti za furaha, hata sauti za wachumba wa kiume na wa kike, tena sauti zao wasemao: Mshukuruni Bwana Mwenye vikosi, ya kuwa Bwana ni mwema! Ya kuwa upole wake ni wa kale na kale! Watavileta vipaji vyao vya kumshukuru katika Nyumba ya Bwana, kwani nitayafungua mafungo ya nchi hii, iwe, kama ilivyokuwa mwanzo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
itasikilikana tena sauti ya furaha na sauti ya shangwe, sauti ya bwana arusi na sauti ya bibi arusi, sauti yao wasemao Mshukuruni BWANA wa majeshi, maana BWANA ni mwema, rehema zake ni za milele; na sauti zao waletao sadaka za shukrani nyumbani kwa BWANA. Kwa kuwa nitawarudisha wafungwa wa nchi hii kama kwanza, asema BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
sauti za arusi na za furaha, sauti za waimbaji wakati wanaleta sadaka za shukrani katika nyumba ya Yawe. Wataimba hivi: Mumushukuru Yawe wa majeshi kwa sababu Yawe ni muzuri, kwa maana wema wake unadumu milele. Nitairudishia inchi hii hali yake ya zamani. –Ni Yawe anayesema.