Jeremiah 33:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: “Mahali hapa ambapo ni jangwa bila watu wala wanyama, na katika miji yake yote, patakuwa na malisho ambayo wachungaji watalisha makundi yao ya kondoo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: ‘Mahali hapa, palipo ukiwa, bila wanadamu wala wanyama: katika miji yake, yatakuwa tena malisho ya wachungaji kuyalaza makundi yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana wa majeshi asema hivi, Katika mahali hapa, palipo ukiwa, hapana mwanadamu wala mnyama, na katika miji yake yote, yatakuwapo makao ya wachungaji wakizilaza kondoo zao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: “Mahali hapa ambapo ni jangwa bila watu wala wanyama, na katika miji yake yote, patakuwa na malisho ambayo wachungaji watalisha makundi yao ya kondoo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu Zote: ‘Mahali hapa, ambapo ni ukiwa pasipo na wanadamu wala wanyama, katika miji yake, patakuwepo tena malisho kwa ajili ya wachungaji kupumzisha makundi yao ya kondoo na mbuzi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Hili ndilo asemalo bwana Mwenye Nguvu Zote: ‘Mahali hapa, ambapo ni ukiwa, pasipo na wanadamu wala wanyama: katika miji yake, patakuwepo tena malisho kwa ajili ya wachungaji kupumzisha makundi yao ya kondoo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA wa majeshi asema hivi, Katika mahali hapa, palipo ukiwa, hapana mwanadamu wala mnyama, na katika miji yake yote, yatakuwapo makao ya wachungaji wakiwalaza kondoo wao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: “Mahali hapa ambapo ni jangwa bila watu wala wanyama, na katika miji yake yote, patakuwa na malisho ambayo wachungaji watalisha makundi yao ya kondoo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema: Mahali hapa palipo Penye mavunjiko, kwa kuwa hapana mtu wala nyama, napo penye miji yake yote patakuwa tena na malisho ya wachungaji, wanapowapumzisha kondoo wao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA wa majeshi asema hivi, Katika mahali hapa, palipo ukiwa, hapana mwanadamu wala mnyama, na katika miji yake yote, yatakuwapo makao ya wachungaji wakizilaza kondoo zao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe wa majeshi anasema hivi: Pahali hapa ambapo ni jangwa bila watu wala nyama, na katika miji yake yote, patakuwa shamba ambalo wachungaji watakulisha ndani yake makundi yao ya kondoo.