Jeremiah 33:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati huo nchi ya Yuda itaokolewa na mji wa Yerusalemu utakuwa salama. Na mji huo utaitwa ‘Mwenyezi-Mungu ni Ukombozi Wetu’.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika siku hizo, Yuda ataokolewa na Yerusalemu ataishi salama. Hili ndilo jina atakaloitwa: Mwenyezi Mungu ni Haki Yetu.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Katika siku zile Yuda ataokolewa, na Yerusalemu utakaa salama, na jina lake atakaloitwa ni hili, Bwana ni haki yetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati huo nchi ya Yuda itaokolewa na mji wa Yerusalemu utakuwa salama. Na mji huo utaitwa ‘Mwenyezi-Mungu ni Ukombozi Wetu’.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika siku hizo, Yuda ataokolewa na Yerusalemu ataishi salama. Hili ndilo jina atakaloitwa: BWANA Ndiye Haki Yetu.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika siku hizo, Yuda ataokolewa na Yerusalemu ataishi salama. Hili ndilo jina atakaloitwa: bwana Haki Yetu.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Katika siku zile Yuda ataokolewa, na Yerusalemu utakaa salama, na jina lake atakaloitwa ni hili, BWANA ni haki yetu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati huo nchi ya Yuda itaokolewa na mji wa Yerusalemu utakuwa salama. Na mji huo utaitwa ‘Mwenyezi-Mungu ni Ukombozi Wetu’.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku zile ndipo, nchi ya Yuda itakapookolewa, nao mji wa Yerusalemu utakaa salama, nalo jina, utakaloitwa ni hili: Bwana ni wongofu wetu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Katika siku zile Yuda ataokolewa, na Yerusalemu utakaa salama, na jina lake atakaloitwa ni hili, BWANA ni haki yetu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati huo inchi ya Yuda itaokolewa na Yerusalema utakuwa salama. Na muji huo utaitwa “Yawe ni Ukombozi Wetu”.