Jeremiah 33:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kadhalika nao makuhani wa ukoo wa Lawi watakuwapo daima kunihudumia wakinitolea sadaka za kuteketezwa na sadaka za nafaka na kunitolea tambiko milele.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
wala makuhani, ambao ni Walawi, kamwe hawatakosa mtu wa kusimama mbele zangu daima ili kutoa sadaka za kuteketezwa, sadaka ya nafaka, na dhabihu.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wala makuhani Walawi hawatakosa kuwa na mtu wa kusimama mbele zangu, na kutoa sadaka za kuteketezwa, na kufukiza matoleo, na kufanya dhabihu daima.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kadhalika nao makuhani wa ukoo wa Lawi watakuwapo daima kunihudumia wakinitolea sadaka za kuteketezwa na sadaka za nafaka na kunitolea tambiko milele.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
wala hata makuhani, ambao ni Walawi, kamwe hawatakosa mtu wa kusimama mbele zangu daima ili kutoa sadaka za kuteketezwa, ili kuteketeza sadaka ya nafaka na kutoa dhabihu.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
wala hata makuhani, ambao ni Walawi, kamwe hawatakosa mtu wa kusimama mbele zangu daima ili kutoa sadaka za kuteketezwa, ili kuteketeza sadaka ya nafaka na kutoa dhabihu.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wala makuhani Walawi hawatakosa kuwa na mtu wa kusimama mbele zangu, na kutoa sadaka za kuteketezwa, na kufukiza matoleo, na kufanya dhabihu daima.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kadhalika nao makuhani wa ukoo wa Lawi watakuwapo daima kunihudumia wakinitolea sadaka za kuteketezwa na sadaka za nafaka na kunitolea tambiko milele.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hata kwao watambikaji na Walawi hatakoseka mtu wa kutumikia usoni pangu, kama ni kuteketeza ng'ombe za tambiko au kuvukiza vipaji vya tambiko au kuyatengeneza matoleo ya tambiko ya kila siku.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wala makuhani Walawi hawatakosa kuwa na mtu wa kusimama mbele zangu, na kutoa sadaka za kuteketezwa, na kufukiza matoleo, na kufanya dhabihu daima.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vilevile nao makuhani wa ukoo wa Lawi watakuwa pale siku zote kwa kunitumikia wakinitolea sadaka za kuteketezwa na sadaka za unga na kunitolea sadaka milele.