Jeremiah 33:26 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, ndivyo ilivyo pia: Sitawatupa wazawa wa Yakobo na Daudi, mtumishi wangu; nitamteua mmoja wa wazawa wake atawale wazawa wa Abrahamu, Isaka na Yakobo. Kwa maana nitawarudishia fanaka yao na kuwahurumia.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
basi nitawakataa wazao wa Yakobo na Daudi mtumishi wangu, na sitachagua mmoja wa wanawe kutawala wazao wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Kwa maana nitawarudisha kutoka nchi ya kutekwa kwao na kuwaonea huruma.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ndipo nitawatupilia mbali wazao wa Yakobo, na Daudi, mtumishi wangu, hata nisitwae wazao wake watawale juu ya wazao wa Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo; kwa maana nitawarudisha wafungwa wao, nami nitawarehemu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, ndivyo ilivyo pia: sitawatupa wazawa wa Yakobo na Daudi, mtumishi wangu; nitamteua mmoja wa wazawa wake atawale wazawa wa Abrahamu, Isaka na Yakobo. Kwa maana nitawarudishia fanaka yao na kuwahurumia.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
basi nitawakataa wazao wa Yakobo na Daudi mtumishi wangu na sitachagua mmoja wa wanawe kutawala juu ya wazao wa Abrahamu, Isaki na Yakobo. Kwa maana nitawarudisha kutoka kwenye nchi ya kutekwa kwao na kuwaonea huruma.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
basi nitawakataa wazao wa Yakobo na Daudi mtumishi wangu, na sitachagua mmoja wa wanawe kutawala juu ya wazao wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Kwa maana nitawarudisha kutoka nchi ya kutekwa kwao na kuwaonea huruma.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ndipo nitawatupilia mbali wazao wa Yakobo, na Daudi, mtumishi wangu, hata nisitwae wazao wake watawale juu ya wazao wa Abrahamu, na Isaka, na Yakobo; kwa maana nitawarudisha wafungwa wao, nami nitawarehemu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, ndivyo ilivyo pia: Sitawatupa wazawa wa Yakobo na Daudi, mtumishi wangu; nitamteua mmoja wa wazawa wake atawale wazawa wa Abrahamu, Isaka na Yakobo. Kwa maana nitawarudishia fanaka yao na kuwahurumia.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Vilevile sitawatupa walio wa kizazi cha Yakobo na cha Dawidi, wala sitaacha kuchukua katika kizazi chake watakaowatawala walio wa kizazi cha Aburahamu na cha Isaka na cha Yakobo, kwani nitayafungua mafungo yao nitakapowahurumia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ndipo nitawatupilia mbali wazao wa Yakobo, na Daudi, mtumishi wangu, hata nisitwae wazao wake watawale juu ya wazao wa Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo; kwa maana nitawarudisha wafungwa wao, nami nitawarehemu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, ndivyo inavyokuwa vilevile: sitawatupa wazao wa Yakobo na Daudi, mutumishi wangu; nitamuchagua mumoja kati ya wazao wake atawale wazao wa Abrahamu, Isaka na Yakobo. Kwa maana nitawarudishia tena hali yao na kuwahurumia.