Jeremiah 33:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana, mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, nasema kwamba nyumba za mji wa Yerusalemu na nyumba za wafalme wa Yuda zitabomolewa kwa sababu ya kuzingirwa na kwa sababu ya mashambulizi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, asemalo kuhusu nyumba zilizo mji huu na majumba ya kifalme ya Yuda, zote ambazo zimebomolewa ili zitumiwe kupinga kuzingirwa na jeshi na dhidi ya upanga
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana Bwana, Mungu wa Israeli asema hivi, katika habari za nyumba za mji huu, na katika habari za nyumba za wafalme wa Yuda, zilizobomolewa ili kuyapinga maboma na upanga;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana, mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, nasema kwamba nyumba za mji wa Yerusalemu na nyumba za wafalme wa Yuda zitabomolewa kwa sababu ya kuzingirwa na kwa sababu ya mashambulizi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana hili ndilo BWANA, Mungu wa Israeli, asemalo kuhusu nyumba katika mji huu na majumba ya kifalme ya Yuda yaliyobomolewa yatumiwe dhidi ya kule kuzungukwa na jeshi na upanga
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana hili ndilo bwana, Mungu wa Israeli, asemalo kuhusu nyumba katika mji huu na majumba ya kifalme ya Yuda yaliyobomolewa ili yatumiwe dhidi ya kule kuzungukwa na jeshi na upanga
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana BWANA, Mungu wa Israeli asema hivi, kuhusu nyumba za mji huu, na kuhusu nyumba za wafalme wa Yuda, zilizobomolewa ili kuyapinga maboma na upanga;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana, mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, nasema kwamba nyumba za mji wa Yerusalemu na nyumba za wafalme wa Yuda zitabomolewa kwa sababu ya kuzingirwa na kwa sababu ya mashambulizi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani hivi ndivyo, Bwana Mungu wa Isiraeli anavyosema kwa ajili ya nyumba za mji huu na kwa ajili ya nyumba za wafalme wa Yuda zilizobomolewa, zitumike kujenga maboma ya kuzuilia panga;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana BWANA, Mungu wa Israeli asema hivi, katika habari za nyumba za mji huu, na katika habari za nyumba za wafalme wa Yuda, zilizobomolewa ili kuyapinga maboma na upanga;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maana Yawe, Mungu wa Israeli, anasema hivi juu ya nyumba za Yerusalema na nyumba za wafalme wa Yuda zilizobomolewa kwa sababu ya vita.