Jeremiah 34:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Neno la Mwenyezi-Mungu lilimjia Yeremia wakati Nebukadneza, mfalme wa Babuloni, pamoja na jeshi lake lote na falme zote za dunia zilizokuwa chini yake, kadhalika na watu wote walipokuwa wakiushambulia mji wa Yerusalemu na miji mingine yote ya kandokando yake:
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati Nebukadneza mfalme wa Babeli na jeshi lake lote, pamoja na falme zote na mataifa katika himaya aliyotawala walikuwa wakipigana dhidi ya Yerusalemu pamoja na miji yote iliyoizunguka, neno hili lilimjia Yeremia kutoka kwa Mwenyezi Mungu:
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa Bwana, hapo Nebukadreza, mfalme wa Babeli, na jeshi lake lote, na falme zote za dunia zilizokuwa chini ya mamlaka yake, na kabila zote za watu, walipopigana na Yerusalemu, na miji yake yote, kusema,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Neno la Mwenyezi-Mungu lilimjia Yeremia wakati Nebukadneza, mfalme wa Babuloni, pamoja na jeshi lake lote na falme zote za dunia zilizokuwa chini yake, kadhalika na watu wote walipokuwa wakiushambulia mji wa Yerusalemu na miji mingine yote ya kandokando yake:
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati Nebukadneza mfalme wa Babeli na jeshi lake lote pamoja na falme zote na mataifa katika himaya aliyotawala walipokuwa wakipigana dhidi ya Yerusalemu pamoja na miji yote inayoizunguka, neno hili lilimjia Yeremia kutoka kwa BWANA:
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati Nebukadneza mfalme wa Babeli na jeshi lake lote, pamoja na falme zote na mataifa katika himaya aliyotawala walipokuwa wakipigana dhidi ya Yerusalemu pamoja na miji yote inayoizunguka, neno hili lilimjia Yeremia kutoka kwa bwana:
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa BWANA, hapo Nebukadneza, mfalme wa Babeli, na jeshi lake lote, na falme zote za dunia zilizokuwa chini ya mamlaka yake, na makabila yote ya watu, walipopigana na Yerusalemu, na miji yake yote, kusema,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Neno la Mwenyezi-Mungu lilimjia Yeremia wakati Nebukadneza, mfalme wa Babuloni, pamoja na jeshi lake lote na falme zote za dunia zilizokuwa chini yake, kadhalika na watu wote walipokuwa wakiushambulia mji wa Yerusalemu na miji mingine yote ya kandokando yake:
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hili ndilo neno lililomjia Yeremia likitoka kwa Bwana, Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, na vikosi vyake vyote na watu wa nchi zote za kifalme, mkono wake ulizozitawala, hayo makabila yote walipopiga vita, wauteke Yerusalemu na miji yake yote, likawa la kwamba:
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa BWANA, hapo Nebukadreza, mfalme wa Babeli, na jeshi lake lote, na falme zote za dunia zilizokuwa chini ya mamlaka yake, na kabila zote za watu, walipopigana na Yerusalemu, na miji yake yote, kusema,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe akamutolea Yeremia ujumbe huu wakati Nebukadneza, mufalme wa Babeli, pamoja na waaskari wake wote na falme zote za dunia zilizokuwa chini ya utawala wake, vilevile na watu wote walipokuwa wakiushambulia Yerusalema na miji mingine yote ya kandokando yake: