Jeremiah 34:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Viongozi wote na watu wote waliofanya agano hilo walikubaliana wote wawaachie huru watumwa wao wa kiume na wa kike, na mtu yeyote asiwafanye tena kuwa watumwa. Walikubaliana, wakawaacha huru.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo maafisa wote na watu walioingia katika agano hili wakakubali kwamba watawaacha huru watumwa wao wa kiume na wa kike, na hawatawashikilia tena. Wakakubali na wakawaacha huru.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na wakuu wote, na watu wote, wakati, waliofanya agano hilo, ya kwamba kila mtu amweke huru mtumwa wake na mjakazi wake, mtu ye yote asiwatumikishe tena; wakatii, wakawaacha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Viongozi wote na watu wote waliofanya agano hilo walikubaliana wote wawaachie huru watumwa wao wa kiume na wa kike, na mtu yeyote asiwafanye tena kuwa watumwa. Walikubaliana, wakawaacha huru.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo maafisa wote na watu walioingia katika agano hili wakakubali kwamba watawaacha huru watumwa wao wa kiume na wa kike na hawatawashikilia tena kama watumwa. Wakakubali na wakawaacha huru.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo maafisa wote na watu walioingia katika agano hili wakakubali kwamba watawaacha huru watumwa wao wa kiume na wa kike, na hawatawashikilia tena kama watumwa. Wakakubali na wakawaacha huru.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na wakuu wote, na watu wote, wakati, waliofanya agano hilo, ya kwamba kila mtu amweke huru mtumwa wake na mjakazi wake, mtu yeyote asiwatumikishe tena; wakatii, wakawaacha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Viongozi wote na watu wote waliofanya agano hilo walikubaliana wote wawaachie huru watumwa wao wa kiume na wa kike, na mtu yeyote asiwafanye tena kuwa watumwa. Walikubaliana, wakawaacha huru.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakayasikia wakuu wote nao watu wote walioingia katika agano hilo la kwamba: Kila mtu ampe mtumwa wake na kijakazi wake ruhusa, wajiendee tu, asiwatumikishe tena kazi za kitumwa; nao walipoyasikia, wakawapa ruhusa, wajiendee tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na wakuu wote, na watu wote, wakati, waliofanya agano hilo, ya kwamba kila mtu amweke huru mtumwa wake na mjakazi wake, mtu ye yote asiwatumikishe tena; wakatii, wakawaacha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakubwa wote na watu wote waliofanya agano hilo walikubaliana wote wawaachilie huru watumwa wao na wajakazi, na mutu yeyote asiwafanye tena kuwa watumwa. Walikubaliana, wakawaacha huru.