Jeremiah 34:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini baadaye walibadili nia zao, wakawashika tena watumwa hao wa kiume na wa kike ambao walikuwa wamewaacha huru, wakawafanya watumwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini baadaye wakabadili mawazo yao, na kuwarudisha wale watumwa waliokuwa wamewaacha huru, wakawafanya tena watumwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini baadaye wakaghairi, wakawarudisha watumwa wale, na wajakazi wale, ambao wamewaacha huru, nao wakawatia utumwani wawe watumwa na wajakazi wao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini baadaye walibadili nia zao, wakawashika tena watumwa hao wa kiume na wa kike ambao walikuwa wamewaacha huru, wakawafanya watumwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini baadaye wakabadili mawazo yao na kuwarudisha wale watumwa waliokuwa wamewaacha huru na kuwafanya tena watumwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini baadaye wakabadili mawazo yao, na kuwarudisha wale watumwa waliokuwa wamewaacha huru, wakawafanya tena watumwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini baadaye wakaghairi, wakawarudisha watumwa wale, na wajakazi wale, ambao wamewaacha huru, nao wakawatia utumwani wawe watumwa na wajakazi wao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini baadaye walibadili nia zao, wakawashika tena watumwa hao wa kiume na wa kike ambao walikuwa wamewaacha huru, wakawafanya watumwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini walipokwisha kufanya hivyo wakawarudia, wakawarudisha watumwa na vijakazi, waliowapa ruhusa, wajiendee tu, wakawashurutisha tena kuwa watumwa na vijakazi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini baadaye wakaghairi, wakawarudisha watumwa wale, na wajakazi wale, ambao wamewaacha huru, nao wakawatia utumwani wawe watumwa na wajakazi wao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kisha walibadilisha nia zao, wakawashika tena watumwa na wajakazi hao ambao walikuwa wamewaacha huru, wakawafanya watumwa.