Jeremiah 34:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
‘Kila mwaka wa saba, kila mmoja wenu atamwacha huru ndugu yake Myahudi aliyeuzwa akawa mtumwa kwa muda wa miaka sita. Mnapaswa kuwaacha huru, wasiwatumikie tena.’ Lakini wazee wenu hawakunisikiliza wala kunitegea sikio.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
‘Kila mwaka wa saba, kila mmoja wenu ni lazima amwache huru mtumwa ambaye ni Mwebrania mwenzenu aliyejiuza kwenu. Baada ya kukutumikia kwa miaka sita, ni lazima umwache huru aende zake.’ Hata hivyo baba zenu hawakunisikiliza wala kunijali.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mwisho wa kila mwaka wa saba kila mtu na amweke huru ndugu yake aliye Mwebrania, aliyeuzwa kwako na kukutumikia miaka sita utamwacha atoke kwako huru, lakini baba zenu hawakunisikiliza, wala hawakutega masikio yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
‘Kila mwaka wa saba, kila mmoja wenu atamwacha huru ndugu yake Myahudi aliyeuzwa akawa mtumwa kwa muda wa miaka sita. Mnapaswa kuwaacha huru, wasiwatumikie tena.’ Lakini wazee wenu hawakunisikiliza wala kunitegea sikio.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
‘Kila mwaka wa saba kila mmoja wenu ni lazima amwache huru mtumwa ambaye ni Mwebrania mwenzenu aliyejiuza mwenyewe kwenu. Baada ya kukutumikia kwa miaka sita, ni lazima umwache huru aende zake.’ Hata hivyo baba zenu hawakunisikiliza wala kunijali.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
‘Kila mwaka wa saba, kila mmoja wenu ni lazima amwache huru mtumwa ambaye ni Mwebrania mwenzenu aliyejiuza kwenu. Baada ya kukutumikia kwa miaka sita, ni lazima umwache huru aende zake.’ Hata hivyo baba zenu hawakunisikiliza wala kunijali.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mwisho wa kila mwaka wa saba kila mtu na amwache huru ndugu yake aliye Mwebrania, aliyeuzwa kwako na kukutumikia miaka sita utamwacha atoke kwako huru, lakini baba zenu hawakunisikiliza, wala hawakutega masikio yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
‘Kila mwaka wa saba, kila mmoja wenu atamwacha huru ndugu yake Myahudi aliyeuzwa akawa mtumwa kwa muda wa miaka sita. Mnapaswa kuwaacha huru, wasiwatumikie tena.’ Lakini wazee wenu hawakunisikiliza wala kunitegea sikio.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwisho wa miaka saba, kila mtu akiwa na ndugu yake wa Kiebureo aliyenunuliwa nawe, sharti umpe ruhusa, atoke kwako, ajiendee tu. Akutumikie miaka sita, kisha sharti umpe ruhusa, atoke kwako, ajiendee tu! Lakini baba zenu hawakunisikia, wala hawakuyatega masikio yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mwisho wa kila mwaka wa saba kila mtu na amweke huru ndugu yake aliye Mwebrania, aliyeuzwa kwako na kukutumikia miaka sita utamwacha atoke kwako huru, lakini baba zenu hawakunisikiliza, wala hawakutega masikio yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kila mwaka wa saba, kila mumoja wenu atamwachilia huru ndugu yake Muyuda aliyeuzishwa kuwa mutumwa kwa muda wa miaka sita. Munapaswa kuwaachilia huru, wasiwatumikie tena. Lakini babu zenu hawakunisikiliza wala kunitegea sikio.