Jeremiah 34:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo, mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nyinyi hamkunitii kuhusu kuwapatia uhuru ndugu zenu Waisraeli. Basi, nami pia nitawapatieni uhuru; uhuru wa kuuawa kwa upanga vitani, kuuawa kwa maradhi na kwa njaa. Nitawafanya muwe kioja kwa falme zote duniani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kwa hiyo, hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Hamkunitii mimi. Hamkutangaza uhuru kwa ndugu zenu. Hivyo sasa, ninawatangazia ninyi ‘uhuru,’ asema Mwenyezi Mungu: ‘uhuru’ ili kuanguka kwa upanga, tauni na njaa. Nitawafanya mwe chukizo kwa falme zote za dunia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Bwana asema hivi, Hamkunisikiliza kumtangazia uhuru kila mtu ndugu yake, na kila mtu jirani yake; tazama, mimi nawatangazieni uhuru, asema Bwana, yaani, wa upanga, na njaa, na tauni; nami nitawatoa ninyi mtupwe huko na huko katika falme zote za dunia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo, mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nyinyi hamkunitii kuhusu kuwapatia uhuru ndugu zenu Waisraeli. Basi, nami pia nitawapatieni uhuru; uhuru wa kuuawa kwa upanga vitani, kuuawa kwa maradhi na kwa njaa. Nitawafanya muwe kioja kwa falme zote duniani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kwa hiyo, hili ndilo asemalo BWANA, hamkunitii mimi, hamkutangaza uhuru kwa ajili ya watu wa kwenu. Hivyo sasa, ninawatangazia ninyi ‘uhuru,’ asema BWANA, ‘uhuru’ ili kuanguka kwa upanga, tauni na njaa. Nitawafanya muwe chukizo kwa falme zote za dunia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kwa hiyo, hili ndilo asemalo bwana: Hamkunitii mimi. Hamkutangaza uhuru kwa ndugu zenu. Hivyo sasa, ninawatangazia ninyi ‘uhuru,’ asema bwana: ‘uhuru’ ili kuanguka kwa upanga, tauni na njaa. Nitawafanya mwe chukizo kwa falme zote za dunia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi BWANA asema hivi, Hamkunisikiliza kumtangazia uhuru kila mtu ndugu yake, na kila mtu jirani yake; tazama, mimi nawatangazieni uhuru, asema BWANA, yaani, wa upanga, na njaa, na tauni; nami nitawatoa ninyi mtupwe huku na huko katika falme zote za dunia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo, mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nyinyi hamkunitii kuhusu kuwapatia uhuru ndugu zenu Waisraeli. Basi, nami pia nitawapatieni uhuru; uhuru wa kuuawa kwa upanga vitani, kuuawa kwa maradhi na kwa njaa. Nitawafanya muwe kioja kwa falme zote duniani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kweli hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Hamkunisikia mkimtangazia kila mtu ndugu yake na mwenzake ukombozi. Kwa hiyo ndivyo, asemavyo Bwana: Mtaniona nikiwatangazia ukombozi na kuwaitia panga na magonjwa mabaya na njaa, nitawatoa ninyi, mtupwe huko na huko katika nchi zote zenye wafalme huku nchini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi BWANA asema hivi, Hamkunisikiliza kumtangazia uhuru kila mtu ndugu yake, na kila mtu jirani yake; tazama, mimi nawatangazieni uhuru, asema BWANA, yaani, wa upanga, na njaa, na tauni; nami nitawatoa ninyi mtupwe huko na huko katika falme zote za dunia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo, Yawe anasema hivi: Ninyi hamukunitii juu ya kuwapatia wandugu zenu Waisraeli uhuru. Basi, nami vilevile nitawapatia ninyi uhuru: uhuru wa kuuawa kwa upanga katika vita, kuuawa kwa ugonjwa mukali na kwa njaa. Nitawafanya ninyi kuwa kitambulisho cha kuogopesha kwa falme zote katika dunia.